*******************************
TAARIFA YA KIFO.
Mnamo tarehe 14.12.2020 majira ya saa 19:00 usiku huko Mtaa wa Isisi uliopo Kata na Tarafa ya Rujewa, Wilaya ya Mbarali, Mwanafunzi wa darasa la tatu katika Shule ya Msingi Uhamila GILISON NGUNGULU [08] alifariki dunia baada ya kuangukiwa na ukuta wa jengo la kanisa la GMCL.
Chanzo cha tukio hilo ni kunyesha kwa mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali hali iliyopelekea ukuta wa jengo hilo kuanguka wakati mtoto huyo akicheza eneo na watoto wenzake ambao hawakupata madhara yoyote katika tukio hilo. Mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi wa kitabibu Hospitali ya Wilaya ya Mbarali na kukabidhi ndugu.
Ninatoa wito kwa wazazi na walezi kuendelea kuchukua tahadhari kwa watoto wao hasa katika kipindi hiki cha mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali kwa kuhakikisha hawachezi maeneo hatarishi na wanakuwa na waangalizi ili kuepuka matukio kama haya. Aidha ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha anafunika visima vilivyo wazi, mashimo kwani ni hatari endapo yatajaa maji.
KUKAMATA MALI ZA WIZI.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limefanikiwa kukamata mali mbalimbali za wizi katika msako uliofanyika tarehe 14.12.2020 majira ya saa 03:46 usiku huko Kijiji na Kata ya Iwindi, Tarafa ya Usongwe, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Mkoa wa Mbeya.
Katika msako huo mali zilizokamatwa ni:-
- Bajaji aina ya TVS King isiyokuwa na namba za usajili
- Kompyuta aina ya Dell – 01,
- Monitor aina ya HP -01,
- Keyboard – 01,
- Shipadoo,
- Mouse 01,
- Extention Cable,
- Radio 01 JVC,
- Sub-Woofer 01 aina ya Jec,
- Speaker 01 kubwa iliyotengenezwa kienyeji,
- Begi 01 dogo ndani yake likiwa na Extention cable 01, Machine 02 za kunyolea nywele, Home Cut pamoja na Msumeno wa kukatia nyama.
Jeshi la Polisi linaendelea na msako wa kuwatafuta watuhumiwa ambao walikimbia na kutelekeza Bajaji na mali hizo. Aidha baadhi ya mali hizo zimetambuliwa na ndugu IMANI MWILE.
KUKAMATWA WATUHUMIWA WA MATUKIO YA KUVUNJA NYUMBA NA KUIBA.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa watano 1. ZAWADI ADIMIN [23] 2. WILLE EMMANUEL [31] 3. HANS LANDA [26] 4. MICHAEL LAURENT [32] na 5. MICHAEL EMANUEL [21] wote wakazi wa Mtakuja katika Mji Mdogo wa Mbalizi kwa tuhuma za kosa la kuvunja nyumba usiku na kuiba mali mbalimbali.
Ni kwamba mnamo tarehe 10.12.2020 majira ya saa 21:00 usiku huko Mtakuja Mbalizi watuhumiwa walivunja mlango wa FREDRICK SHITUNDU na kisha kuiba Televisheni moja, Deck, Godoro, Radio na Remote Control vyote vikiwa na thamani ya Tshs.1,204,450/=.
Kutokana na tukio hilo, Jeshi la Polisi lilianza msako na mnamo tarehe 14.12.2020 lilifanikiwa kuwakamata watuhumiwa watano wakiwa na Radio, TV na Godoro. Watuhumiwa wamehojiwa na kukiri kuhusika katika tukio hilo. Mali zote zimetambuliwa na mlalamikaji. Watuhumiwa watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi wa shauri hili kukamilika.
KUKAMATWA MTUHUMIWA WA MATUKIO YA WIZI.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia ERICK JUMA [31] Mkazi wa Mazimbo Wilaya ya Chunya kwa tuhuma za makosa ya kuvunja nyumba usiku na kuiba pamoja na kupatikana na mali za wizi.
Mtuhumiwa alikamatwa mnamo tarehe 13.12.2020 majira ya saa 11:00 asubuhi huko Kijiji na Kata ya Isangawana, Tarafa ya Kipembawe, Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya. Katika upekuzi uliofanyika nyumbani kwa mtuhumiwa alikutwa mali za wizi zifuatavyo:-
- TV aina ya Home Tec inchi 24.
- Simu ndogo aina ya Tecno.
- Smart Phone aina ya Tecno.
- Extension Cable moja.
Mtuhumiwa amekiri kuiba mali hizo nyumbani kwa ndugu NICOLAUS COSMAS tarehe 22.11.2020 baada ya kuvunja nyumba ya mhanga.
KUPATIKANA NA BIDHAA ZILIZOPIGWA MARUFUKU NCHINI.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia SANDE JOSEPH [24] Mkazi wa Mshikamano Mji Mdogo wa Mbalizi akiwa na Pombe kali Ice London Gin katoni 04 zilizopigwa marufuku nchini kutoka nchini Malawi.
Mtuhumiwa alikamatwa mnamo tarehe 11.12.2020 majira ya saa 10:30 asubuhi huko Mtaa wa Mapelele – Tunduma, Kata Nsalala, Tarafa Usongwe, Wilaya ya Kipolisi Mbalizi, Mkoa Mbeya.
KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO].
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia MERINA FANISHA [25] Mkazi wa Sangambi Wilaya ya Chunya akiwa na Pombe haramu ya Moshi [Gongo] lita 07.
Mtuhumiwa alikamatwa mnamo tarehe 12.12.2020 majira ya saa 20:00 usiku huko Kitongoji cha Majengo, Kata ya Sangambi, Tarafa ya Kiwanja, Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya. Mtuhumiwa ni muuzaji na mtumiaji wa Pombe hiyo.
KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] NA KUINGIZA POMBE ZILIZOPIGWA MARUFUKU NCHINI.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia 1. GWANDI MARTINI [24] na 2. OSCAR MATOLA [23] wote wakazi wa Kasyeto wakiwa na Pombe haramu ya Moshi [Gongo] lita 04 na Pombe kali zilizopigwa marufuku nchini aina ya Win chupa 13.
Watuhumiwa walikamatwa mnamo tarehe 12.12.2020 majira ya saa 10:15 asubuhi huko Mtaa wa Mbila, Kata ya Msasani, Tarafa ya Tukuyu mjini, Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya. Watuhumiwa ni wauzaji na watumiaji wa pombe hiyo. Watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.
KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO].
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa wawili 1. RAPHAEL EMMANUEL [49] na EDINA GEOFREY [37] wote wakazi wa Kijiji cha Mpuga Wilaya ya Rungwe wakiwa na Pombe Moshi lita 10.
Watuhumiwa walikamatwa mnamo tarehe 14.12.2020 majira ya saa 13:30 mchana huko Kijiji na Kata ya Kisondela, Tarafa ya Ukukwe, Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya katika misako inayoendelea maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mbeya. Watuhumiwa ni wauzaji wa Pombe hiyo, watafikishwa mahakamani baada ya taratibu kukamilika.
KUKAMATWA MTUHUMIWA WA WIZI WA MIFUGO.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia NANGALI MWAMBA [31] Mkazi wa Makatang’ombe Wilaya ya Chunya kwa tuhuma za kosa la wizi wa Ng’ombe 07 wenye thamani ya Tshs.4,200,000/=.
Awali mnamo mwezi Novemba, 2020 huko Wilaya ya Chunya mtuhumiwa aliiba Ng’ombe hao na kutokomea. Kutokana na tukio hilo Jeshi la Polisi lilianza msako na mnamo tarehe 12.12.2020 majira ya saa 15:30 alasiri huko Kijiji cha Itumbi, Kata ya Matundasi, Tarafa ya Kiwanja, Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya alikamatwa. Upelelezi unaendelea.
KUPATIKANA NA BHANGI.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa wawili 1. HAMIS ADAM [43] Mkazi wa Utengule Usongwe na 2. NDULU MEGALI [37] Mkazi wa Kanioga – Rujewa wakiwa na dawa za kulevya aina ya Bhangi Gramu 500.
Watuhumiwa walikamatwa mnamo tarehe 13.12.2020 majira ya saa 08:45 asubuhi huko Kitongoji cha Wimba, Kijiji na Kata ya Utengule Usangu, Tarafa ya Ilongo, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Mkoa wa Mbeya. Aidha mtuhumiwa NDULU MEGALI [37] anatuhumiwa kwa kosa la kuchoma moto kibanda huko Rujewa Wilaya ya Mbarali. Upelelezi wa mashauri haya unaendelea na mara baada ya kukamilika watuhumiwa watafikishwa mahakamani.
KUPATIKANA NA BHANGI.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia HAMPHREY MAYUNGA [23] Dereva Bajaji na Mkazi wa Mwakibete Jijini Mbeya akiwa na akiwa na dawa za kulevya aina ya bhangi gramu 190.
Mtuhumiwa alikamatwa mnamo tarehe 13.12.2020 majira ya saa 11:45 asubuhi huko maeneo ya Njia panda ya Uwata – Hospitali, Kata ya Mwakibete, Tarafa ya Iyunga, Jiji la Mbeya. Mtuhumiwa ni mtumiaji na muuzaji wa bhangi. Upelelezi unaendelea.