Naibu Waziri Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Kipanga Juma Omary akipokelewa na baadhi ya viongozi wa TET kwaajili ya kutembelea kiwanda cha uchapaji vitabu cha Press A kwa lengo la kuona ujio wa mashine mpya za uchapaji vitabu vya kiada ambazo zitarahishisha zoezi la uchapaji na kuongeza idadi ya vitabu mashuleni. Naibu Waziri Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Kipanga Juma Omary akizungumza baada ya kutembelea kiwanda cha uchapaji vitabu cha Press A kwa lengo la kuona ujio wa mashine mpya za uchapaji vitabu vya kiada ambazo zitarahishisha zoezi la uchapaji na kuongeza idadi ya vitabu mashuleni. Naibu Waziri Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Kipanga Juma Omary akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kiwanda Press A Bw.John Kaswalala (kulia) baada ya kutembelea kiwanda hicho na kujionea utendaji kazi wake.
Naibu Waziri Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Kipanga Juma Omary akipata picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania TET Dkt. Aneth Komba na baadhi ya wafanyakazi wa TET baada ya kutembelea kiwanda cha uchapaji vitabu cha Press A kwa lengo la kuona ujio wa mashine mpya za uchapaji vitabu vya kiada ambazo zitarahishisha zoezi la uchapaji na kuongeza idadi ya vitabu mashuleni.
************************************
NA EMMANUEL MBATILO
Naibu Waziri Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Kipanga Juma Omary ametaka Taasisi ya Elimu Tanzania TET kuhakikisha kuwa wanafanya kazi usiku na mchana kufunga mashine mpya za uchapaji kutokana na kuwa nje ya muda.
Hayo ameyasema leo Jijini Dar es Salaam Naibu Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Mhe.Kipanga alipotembelea kiwanda cha uchapaji vitabu cha Press A kwa lengo la kuona ujio wa mashine mpya za uchapaji vitabu vya kiada ambazo zitarahishisha zoezi la uchapaji na kuongeza idadi ya vitabu mashuleni.
“Tuanze kufunga mitambo hiyo siku ya tarehe 23 lakini kama mitambo hiyo inafungwa ndani basi kazi hiyo iweze kufanyika usiku na mchana maana watu wanaweza kufanya kazi kwa shifti hivyo muda haupo na sisi”. Amesema Mhe.Kipanga Juma.
Aidha amesema amewataka wafanyakazi wa kiwanda hicho kuendelea na utunzaji mzuri wa mashine hizo kutokana na umuhimu wake na gharama za manunuzi kuwa kubwa.
Hata hivyo ameitaka TET kuhakikisha ufungaji wa mashine hizo unaanza Desemba 23 2020 na kumaliza January 2021 ili kuondoa changamoto ya upungufu wa vitabu mashuleni hususani kwa mwaka mpya wa masomo unaoanza mwakani.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania TET Dkt. Aneth Komba amesema wana vituo 5 vya uchapaji nchini ambavyo vinachapa vitabu na Press A imekuwa ikichapa vitabu vyote vya viongozi vya mwalimu kuanzia darasa la 1 hadi viii kwa jumla ya nakala 1,698,595 na maandishi makubwa kwa wenye uoni hafifu 13,500.
Aidha Dkt.Komba amesema pamoja na uchapaji wa vitabu viwanda hivyo huchapa pia nyaraka mbalimbali za serikali ambapo kabla ya kukabidhiwa viwanda hivyo kazi hizo zilikuwa zinafanywa na wachapaji bibafsi.
Hata hivyo amesema ufungwaji wa mitambo hiyo mipya kutasaidia kuongeza ajira, kazi za uchapaji, kupunguza gharama na kurahisisha upatikanaji wa machapisho kwani kwa sasa wachapaji wengi hufanya kazi hizo nje ya nchi.
Dkt. Komba ameongeza kuwa mashine zinazotarajiwa kufungwa ni saba ambapo mchakato wake wa manunuzi ulianza toka mwaka 2017 na mashine ya kwanza ilifika kiwandani Novemba 2019 huku ya mwisho ikifika Desemba 1, 2020.
Amesema kuwa ucheleweshaji wa ufungaji wa mashine hizo umetokana na kuchelewa kuletwa kwa mashine hizo toka kwa mzabuni ambapo mkataba wa nwisho uliongezwa hadi Novemba 15, 2020.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Baraza la TET Prof.Gasto Mapunda amesema jukumu lao ni kuhakikisha kuwa wanaisimamia utendaji kazi wa viwanda hivyo ili vichapishe machapisho yenye tija.
Amesema kwa sasa Taasisi inangalia taratibu za kufunga kampuni ya kibiashara ya uchapaji na watahakikisha kuwa ufungwaji wa mashine hizo unafanya kwa wakati.