Mratibu wa malaria mkoa wa Katavi Emmanuel Kipande kama alivyokutwa na mwandisgi wa haari ofisini kwake.
Mama Devotha Lemi akiwa na mwanawe Richard Magaso wakisubiri huduma katika zahanati ya Ugala.
****************************************
Idara ya Afya ya mkoa wa Katavi inaendelea kufanya jitihada mbalimbali katika kuhakikisha inapunguza ya ugonjwa wa malaria kwa watoto
Mratibu wa malaria mkoa wa katavi bwana Emmanuel Kipande amesema wanapuliza dawa za kuua vimelea vya wadudu wa malaria katika madimbwi ya maji yaliyotuama na mashimo katika maeneo mbalimbali
Aidha bwana Kipande amesema pia wanahimiza usafi wa mazingira katika makazi ya watu sanjari na kuhamasisha watu kutumia vyandarua kwa usahihi
Ameeleza kuwa idadi kubwa ya watoto wanaofika kutibiwa katika zahanati, vituo vya afya na hospitali na kukutwa na malaria wana umri wa kati ya mwaka mmoja hadi nane
Ameendelea kusema kuwa kati ya watoto 1000 waliopimwa malaria kwa mwaka 2020 kati yao watoto 100 walibainika kuwa na malaria tofauti na mwaka 2019 ambapo kati ya watoto 1000 waliopimwa malaria watoto 150 hadi 200 walikutwa na malaria
Halikadhalika wameendelea kuhimiza matumizi ya vyandarua kwa kinamama wajawazito na watoto ambapo wanagawa vyandarua kwa kinamama wajawazito na kinamama wenye watoto wa miezi tisa
Zoezi hilo la ugawaji wa vyandarua pia umefikia hadi katika shule za msingi ambapo watoto wa darasa la pili walipewa vyandarua bure
Kwa kipindi cha Januari – Juni mwaka 2020 vyandarua 67,560 viligawiwa kwa kinamama wenye watoto wenye umri wa miezi tisa waliofika kupata chanjo ya surua; na vyandarua 112,088 viligawiwa kwa shule za msingi 186
Bi. Martha Mwakangale ni mkazi wa kata ya Ugalla halmashauri ya Nsimbo, akizungumzia suala la usafi wa mazingira amesema viongozi wa kata wamekuwa wakiwazungukia wananchi na kuwahimiza kufyeka majani yanayozunguka nyumba
Ameongeza kuwa endapo utakaidi kufanya usafi katika makazi yako utatuzwa faini ya shilingi 20,000/-
Kuhusu kujikinga na malaria amesema familia yake inatumia vyandarua vyenye dawa ambavyo walipewa na serikali