Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe William Lukuvi akisisitiza jambo mbele ya Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoa wa Dar es Salaam wakati wa kupokea Taarifa kutoka Kamati zinazoshughulikia migogoro ya ardhi kwenye maeneo ya Chasimba, Chatembo, Nyakasangwe na Mambwepande jijini Dar es Salaam. Kushoto kwa Lukuvi ni Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Abuubakar Kunenge.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe William Lukuvi akifurahia jambo na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Abuubakar Kunenge (Kulia), Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo (wa pili kushoto) na Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Dar es Salaam Idrisa Kayera (kushoto) wakati wa kikao cha kupokea Taarifa kutoka Kamati zinazoshughulikia Migogoro ya Ardhi kwenye maeneo ya Chasimba, Chatembo, Nyakasangwe na Mambwepande jijini Dar es Salaam. (PICHA NA WIZARA YA ARDHI)