Waziri wa nishati Dkt . Merdad Kalemani katikati akitoa maelekezo kwa mkandarasi wa kituo chakipoozea umeme Kv 400 Lemuguru kilichopo Ndani ya Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha alipotembelea Mradi huo leo (Jana) na kuangalia Mradi huo ulipofikia ambapo aliwataka wafanye kazi usiku na mchana adi ifikapo March 31 ,2021 Mradi huo uwe umekamilika(picha na Woinde Shizza ,ARUSHA)
**********************************
Na Woinde Shizza ,ARUSHA
Waziri wa nishati Dkt. Merdad Kalemani amechukizwa na kitendo Cha kuzorota kwa Mradi wa kituo Cha kupozea umeme kilichopo lemuguru Ndani ya kata ya mateves Wilayani Arumeru mkoani Arusha
Akitembelea Mradi huo Dkt .Kalemani ametoa muda wa miezi mitatu kwa mkandarasi wa kampuni ya consortium Energoinvest &E.M.C LTD ,Irfan Djovic Kuhakikisha Mradi huo unakamilika kwa muda huo aliowapa.
Alisema mradi huu ulianza December 2017 na ulitakiwa ukamilike Ndani ya miaka mitatu, lakini shughuli za Ujenzi rasmi zilinza rasmi mwaka 2018 gharama za Mradi huu ni Dola milioni miambili hamsini na nane pointi mbili ,unajegwa umbali wa kilometa 414 kwa Tanzania na mpaka kufikia upande wa Kenya Naisinyai itakuwa imefikia kilometa 512, laini hii ni muhimu Sana kwa nchi yetu mpaka nchi za jirani.
Aliongeza kuwa mradi huu ulitakiwa ukamilike December 31 mwaka huu lakini alivyotembelea ameona Mradi huo hauta kamilika kwa wakati huo na alivyoongea na mkandarasi amemwambia visingizio ambao avirizishi vikiwemo uwepo wa ugonjwa was Covid 19,uwepo wa mvua visingizio ambavyo ajaridhishwa navyo maana kwanza nchi yetu haina ugonjwa huo na Kama upo mbona wakandarasi wengine wanaendelea na miradi bila visingizio hivyo na hata swala la mvua alisema ametembelea Mradi hiyo na hajaona mvua yoyote hivyo ajakubaliana na kisingizio hicho.
“Nielekeze wafanyakazi waongezwe , pia mkandarasi zile mashine kubwa ambazo zinaagizwa nje kwa ajili ya kituo hichi Cha kupozea umeme mkandarasi ulitaka uanze kuleta vifaa hivyo mwezi January Mimi ninakwambia hapana anza kuingiza kesho ivyo vifaa ili mpaka January viwe vimefika hapa na Mradi huu muakikishe ukamilike mwishoni mwa mwezi March “alisema Kalemani
Aidha alimtaka meneja wa Mradi huo pamoja msaidizi wake ambaye ni muhandisi ampeleke maelezo ndani ya siku tatu kwanini Mradi huo umesimama na wafanyakazi hawapo kazini mpaka Sasa na kwanini Mradi haujakamilika kwa wakati na maelezo hayo akiyasoma asipo rizika nayo inawabidi wajiuzuru.
Kalemani alimtaka meneja wa Shirika la Umeme Tanesco mkoa wa Arusha Hereni mhina pamoja na meneja wa Shirika hilo Wilaya ya Arumeru pamoja na wa Kanda kusimamia wakandarasi wamalize Mradi huo kwa wakati ,huku akiwasisitiza wasiende kula sikujua mpaka pale Mradi utakapo kamilika huku akiwasisitiza wakandarasi wageni kutoka nchi za nje kuzileta familia zao hapa nchini nakusherekea sikukuu pamoja ili wasitafute visingizio vya kusema wanaenda kula sikuku makwao,ambapo pia aliwasisitiza wafanye kazi usiku na mchana ili adi ifikapo mwezi March Mradi uwe umekamilika.
“Umuhimu wa Mradi huu unafanya kazi tatu kazi ya kwanza kujenga laini ya kufikisha umeme lemuguru umbali wa kv 400 ambayo inaendana na kv 220 kazi ya pili inasambaza umeme Katika vijiji 38 ambavyo vipo mikoa ya Singida , Manyara na Arusha kuchelewa kwake kunachelewesha wananchi ambao wapo kwenye laini kupata umeme hivyo ni vyema Mradi huu unakamilika haraka”alisema Kalemani
Muhandisi Msimamizi wa Mradi wa kituo Cha kupozea umeme kituo Cha Lemuguru Blandina Joachim alisema mpaka Sasa Mradi umekamilika kwa Asilimia 60 % ,na hii inatokana na changamoto mbalimbali ambazo wameziainisha lakini Waziri amezikataa lakini pia changamoto kubwa inayowakabili ni ucheleweshaji wa vifaa na ndio imechangia kwa kiasi kikubwa Mradi kutikamilika.
Aidha alisema kuwa wao Kama tanesco wamechukuwa hatua kwa kuanza kubadilisha ankaunti za mkandarasi za nje na kuziamishia hapa Ndani na hawataruhusu Ela zozote kwenda nje ,na hii pia utawasaidia kuangalia matumizo ya fedha izo na jinsi Mradi unavyoenda.