Mbunge wa viti maalum Zaituni Swai akiwa anapima afya yake juzi wakati wa zoezi la kupima magonjwa yasiyoambukizwa lililokuwalikiendelea Katika viawanja vya USA ,Wilayani Arumeru ,zoezi hili limeandaliwa na kampuni ya phide intantament iliopo jijini Arusha (picha na Woinde Shizza ,ARUSHA)
*************************************
Na Woinde Shizza , michuzi Tv -ARUSHA
Mbunge wa viti maalum,Zaituni Swai amewataka wananchi wilayani Arumeru kuzingatia mlo kamili pomoja na kubadili mienendo ya tabia inayochangia kupata magonjwa yasiambukiza ili kupunguza idadi ya magonjwa hayo.
Akizungumza katika zoezi la upimaji wa magonjwa hayo ,kama vile kisukari,kansa,moyo ,macho pamoja na uchangiaji damu lililoratibiwa na kampuni ya phide entertainment kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ,mbunge Swai alisema mtu yeyote mwenye afya bora anauwezo wa kutekeleza shughuli yoyote hivyo ni vyema kuzingatia mlo kamili pamoja na kubadili mienendo ya kitabia.
“Mienendo ya kitabia kama unywaji wa pombe kupitiliza,uvutaji wa sigara na hutumiaji wa madawa ya kulevya huchangia kupata magonjwa yasiyoambukiza hivyo ni vyema kila mwananchi akazingatia afya yake kwa kufuata maelekezo ya wataalam wa afya pamoja na kufanya mazoezi ya viungo,”alisema Mbunge huyo.
Mbunge Swai alisema atashirikiana na mkuu wa wilaya hiyo,Jerry Muro kuhamasisha wananchi wa Arumeru katika zoezi la ufanyaji wa mazoezi kama kuwakumbusha kuwa kwa kufanya hivyo kutasaidia kupunguza idadi ya watu wenye magonjwa yasiyoambukiza.
Kwa upande wake Kaimu mganga mkuu wa wilaya hiyo,Dr.Hillary Mkini alisema magonjwa ya kisukari na kanda yanaweza kuzuilika kwa kubadilisha mienendo ya maisha hivyo ni vyema wananchi wakazingatia mlo kamili pamoja na kufanya mazoezi kila mara kutasaidia mwananchi awe na afya bora nakuweza kutekeleza majukumu yake kwa Taifa.
“Wananchi wajenge tabia ya kupima afya kila mara kwani serikali imeboresha utaratibu wa kujiunga na bima ya afya ili kusaidia kupata matibabu na kupunguza gharama za hospitali,”alisema Kaimu Mganga Mkuu huyo.
Naye Mkurugenzi wa kampuni hiyo iliyoratibu zoezi hilo Phidesia Mwakitalima alisema
zoezi hilo la upimaji tangu kuanza kwake lina muda wa miaka minne na kwani watu wengi huwa wanajitokeza ili kupima afya zao takribani 3500 na kwa upande wa huchangiaji damu huwa wanapata sio chini ya pakti 200 za damu ambazo zinaenda kusaidia wagonjwa kutoka hospitali zilizopo mkoani Arusha.
“Wakazi wa Arusha wamekuwa na mwitikio mkubwa wa zoezi hili kutoka maeneo mbalimbali kwa nia ya kujua afya zao kutokana na magonjwa yasiyoambukizwa kuonekana yanatesa watu hivyo anawashukuru wadhamini wa zoezi hilo zikiwemo radio za mkoa huu na telavisheni
“Na kutokana na huduma hizi mara nyingi sio rahisi kupata bure kwa wakati wote hivyo anaomba wadau mbalimbali waendelee kujitokeza kwa kusaidia jamii katika zoezi la kufanikisha upimaji wa magonjwa yasiyoambukiza,”alisema Mkurungenzi Phide.
Mmoja wa wananchi kutoka wilayani Arusha,Fadira Shayo alisema zoezi hilo limewafikia kwa wakati hivyo anaomba liwe endelevu ili kuweza kuwafikia wagonjwa wale wasioweza kutembea hata katika vitongoji kwani watu wengi hawaendi hospitali kwa kuogopa gharama.
“Mimi nachoamini ni kwamba ukizingatia maelekezo ya wataalamu wa afya magonjwa yasiyoambukiza yatapungua hivyo nashukuru wadau mbalimbali waliofanikisha zoezi hili kwani limetufurahisha,”alisema Shayo.