Ubalozi wa Tanzania nchini Qatar umeanzisha
rasmi programu ya mafunzo kwa waajiriwa wapya kutoka Tanzania wanaokwenda kufanya kazi nchini
humo.
Mafunzo hayo yameanzishwa kwa makubaliano kati ya Ubalozi na Kampuni zote Kadhalika, mafunzo hayo yameanzishwa ili kuwajulisha maadili, mila na utamaduni za Qatar pamoja na kuwahimiza kujua wajibu wao ili kudumisha heshima ya Tanzania kimataifa na kuitangaza vyema nchi. Mafunzo ya awali yametolewa tarehe 12 Desemba, 2020 kwa Mabinti 9 kutoka Tanzania ambao wameajiriwa na Kampuni ya Qatar Manpower Solutions (WISA) inayomilikiwa na Serikali kwa ajili kufanya usafi na huduma za ndani. Mafunzo hayo ambayo yamesimamiwa na Bw. Volka Gowele, Afisa wa Ubalozi yameendeshwa na Bw. Sahim Ayoub Khatib, Diaspora wa Tanzania na Mwajiriwa kwenye |
Bw. Sahim Ayoub Khatib (mwenye karatasi), Diaspora wa Tanzania nchini Qatar ambaye pia ni Mwajiriwa wa Kampuni ya HBK ya nchini humo akitoa mafunzo kwa Mabinti 9 kutoka Tanzania ambao wameaajiriwa na Kampuni ya Manpower Solutions (WISA) inayomilikiwa na Serikali kwa ajili ya kufanya kazi za usafi na huduma za ndani. Mafunzo hayo ambayo yanalenga kuwajengea uwezo pamoja na kuwaelewesha sheria na taratibu za ajira za Qatar, yameandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini humo. Mafunzo hayo yalifanyika kwenye Ofisi za Ubalozi hivi karibuni na kusimamiwa na Bw. Volka Gowele (mwenye barakoa), Afisa wa Ubalozi. |
Mafunzo yakiendelea kwa Mabinti hao |
Mabinti tisa kutoka Tanzania walioshirki mafunzo ya kuwajengea uwezo yaliyoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Qatar |