Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Neema Lugangira (MB) akisisitiza jambo wakati akitoa elimu ye Lishe bora kwa madiwani wa Halmashauri ya Kongwa mkoani Dodoma |
Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Neema Lugangira (MB) akisisitiza jambo wakati akitoa elimu ya Lishe bora kwa madiwani wa Halmashauri ya Kongwa mkoani Dodoma |
Mkurugenzi wa
Taasisi hiyo Neema Lugangira (MB) akisisitiza jambo wakati akitoa elimu
ya Lishe bora kwa madiwani wa Halmashauri ya Kongwa mkoani Dodoma ambao hawapo pichani
MKUU wa wilaya ya Kongwa kulia Dkt Selemani Serera kulia akiwa na Mkurugenzi wa
Taasisi hiyo Neema Lugangira (MB) wa tatu kushoto wakifuatilia kwa umakini michango ya madiwani wakati wa semina ya lishe bora
katikati ni Mkurugenzi Halmashauri wa Kongwa Dkt Omary Nkullo
MKUU
wa wilaya ya Kongwa kulia Dkt Selemani Serera kulia akiteta jambo na
Mkurugenzi wa
Taasisi hiyo Neema Lugangira (MB) wa pili kushoto wakati wa semina ya
lishe bora katikati ni Mkurugenzi Halmashauri wa Kongwa Dkt Omary Nkullo
Sehemu ya madiwani wakifuatilia matukio mbalimbali
MADIWANI wa Halmashauri ya Kongwa wilayani Kongwa Mkoani Dodoma wamekuwa viongozi wa kwanza wa kisiasa hapa nchini kupatiwa elimu ya lishe bora.
Mnamo 2019, Shirika la Agri Thamani Foundation lilianzisha na kuratibu mchakato wa ajenda ya Lishe Bora kuwa kipaumbele na kuingizwa kwenye Ilani za Uchaguzi 2020-2025 za Vyama vya Siasa 3 nchini; Chadema, ACT Wazalendo na Chama Tawala – Chama Cha Mapinduzi.
Baada ya kufanikiwa kuingiza Ajenda ya Lishe katika Ilani za Uchaguzi 2020-2025 za Vyama vyote 3 huku Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ilienda mbali zaidi kwa kuanisha kwa kina malengo yake katika kuimarisha hali ya Lishe nchini, Agri Thamani imeanzisha programu ya kutoa mafunzo ya lishe bora kwa Madiwani.
Programu hii imezinduliwa kwa kutoa mafunzo ya lishe bora kwa mara ya kwanza wilayani Kongwa kwa lengo la kuwapa Madiwani uelewa mpana wa ajenda hii na kuwawezesha kusimamia utekelezaji wake.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango huo wa Elimu ya Lishe Bora; Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Neema Lugangira (MB) alisema wameamua kutoa elimu hiyo ili ikawe chachu kwa jamii kubadiliana na kuondokana na tatizo la lishe kwenye maeneo yao.
Alisema kutokana na kwamba madiwani hao wanaongoza idadi kubwa ya wananchi huku wakiwa na ushawishi mkubwa kwa jamii wanayoiongoza hivyo elimu ya lishe bora itasaidia jamii kuweza kutambua na kuepukana na suala la lishe duni.
Kwa kuanzia Elimu ya Lishe Bora itatolewa kwa Madiwani kwa makundi kutoka Mkoa wa Dodoma, Tabora, Kigoma, Tanga na Kagera.
Awali akizungumza katika uzinduzi huo Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Dkt Selemani Serela aliishukuru Taasisi hiyo kwa kuona umuhimu kwa kutoa elimu kwa madiwani hao na kueleza itakuwa ni chachu ya elimu hiyo kuendelezwa zaidi.
Alisema kwamba wanaomba pia ushirikiano wa elimu ambayo imeitolewa inahitajika iendele zaidi huku akitaka lazima wachukue hatua kwa vitendo ili kuondokana na suala la lishe duni kwenye jamii.
“Lazima tuchukue hatua kwa vitendo, tunategemea tuone namna gani tunaweza kufikia hatua ambazo tumekubaliana hapa na tuwe na mpango kazi unaopimika ”Alisema
Aidha alisema pia leo ilikuwa ni hatua ya kwanza ya kuwasilisha mada hivyo wanategemea kuona mikakati inawekwa ya namna gani wanaweza kufikia hatua ambazo wamekubaliana.
“Tutakaa kama wilaya tuone tunafanyaje madiwani wanafanya kazi kubwa sana tunahitaji wataalamu mnapokuja kila mara kutuongezea uelewa hatua ambayo itasaidia kuibadilisha jamii. Tunahitaji pia Agri Thamani muungane nasi katika jitihada hizi hapa Kongwa “Alisema DC huyo
Naye kwa upande wake Afisa Lishe wa wilaya ya Kongwa Maria Haule alisema wamekuwa wakifanya shughuli wakilenga makundi yaliyopo kwenye hatari kubwa ya kupata changamoto ya lishe duni hasa matunzo yasipokuwa vizuri.
Alisema takwimu zinaonyesha mkoani Dodoma asilimia 37.2 ya watoto chini ya umri wa miaka 5 wana udumavu. Takwimu hizi ni kwa mujibu wa TNNS 2018.
Maria alisema lakini pia takwimu halmashauri za afya zinaonyesha asilimia 24 ya upungufu wa damu na asilimia 0.1 ya ukondefu kwa watoto chini ya miaka mitano.
Alisema wao kama wilaya wana mikakati kukabiliana na hiyo changamoto ikiwemo kutenga fedha kwa ajili ya afua za lishe.
Alieleza huku akitolea mfano kwa mwaka huu wa fedha wametenga milioni 77.5 ambapo hiyo ni kwa mujibu wa Sera ya Serikali kila mtoto aliyechini ya umri wa miaka 5 anatengewa sh 1,000 kwa ajili ya afua za lishe.
Afisa Lishe huyo alisema katika hiyo bajeti ipo inayosaidia kugharamikia matibabu kwa watoto wenye utapiamlo mkali na pia wametenga milioni 32 kwa ajili ya chakula la dawa na vifaa tiba ikiwemo kuwajengea uwezo watoa huduma za afya vituo namna ya kuendelea kuelimisha jamii kwenye masuala la lishe na kutibu wenye watakaonekana wana lishe duni.
Afisa Lishe alisisitiza umuhimu wa Agri Thamani kuwa na ofisi Kongwa ili waweze kushirikiana kwa karibu katika kutokomeza changamoto ya udumavu na utapiamlo kwa ujumla wilayani Kongwa.
Hata hivyo Diwani wa Viti Maalumu (CCM) anayetokea wilaya ya Kongwa Fatuma Diria aliishukuru Agri ThamanI kwa kutoa semina hiyo na kwa kweli wamejifunza mambo mengi mazuri na yenye manufaa kwao na kwa jamii.
Alisema wakati mwengine nilikuwa naelewa lakini nilikwa naona kuna watoto wanasoma shule hawana uwela sikujua kwamba chanzo kinaanzia kwa mama mjamzito kutokana na lishe duni wakati mama akiwa mjamzito .
Hata hivyo alisema kwa kupata elimu hiyo atakwenda kuwa balozi wa kuihamasisha jamii kuhakikisha inachukua hatua za kukabiliana na tatizo hilo kwa kupata lishe bora.
Kwa upande wake, Mkurugezi wa Halmashauri ya Kongwa Dkt Omary Nkullo ameishukuru sana Agri Thamani kwa kuanzia Kongwa na ameahidi Kongwa itakuwa Halmashauri ya Mfano kwenye Lishe. Alimalizia kwa kuikaribisha sana Agri Thamani Kongwa ili wafanye kazi pamoja.