Baadhi ya wananchi wa Wilaya ya uyui wakiwa katika sherehe za uzinduzi wa Baraza jipya la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui.
Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu akitoa maelezo mafupi wakati uzinduzi wa Baraza jipya la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya UyuI
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati akitoa maelezo wakati wa uzinduzi wa Baraza jipya la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui Said Ntahondi akifunga kikao cha kwanza cha Baraza la Madiwani mara baada ya kuzinduliwa .
Katibu Tawala Wilaya ya Uyui Moses Pesha akitangaza matokeo ya uchaguzi wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui Hemed Magaro akitoa maelezo wakati wa kikao cha kwanza cha uzinduzi wa baraza jipya la Madiwani wa Halmashauri hiyo.
PICHA NA TIGANYA VINCENT
******************************************
NA TIGANYA VINCENT
MKUU wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati amewataka Madiwani kuhakikisha wanasimamia Watendaji wa vijiji ili wajenge utamaduni wa kusoma taarifa za mapato na matumizi kwa wananchi wao kila baada ya robo yam waka ili kuondoa migogoro.
Hatua hiyo itasaidia kuondoa migogoro ya wananchi kukataa kuchangia fedha katika miradi yao ya maendeleo kwa kuhofia kuwa michango yao inatafunwa na viongozi wa vijiji vyao
Dkt. Sengati alisema hayo jana wakati akitoa hotuba ya uzinduzi wa Baraza jipya la Halmashauri ya Wilaya ya Uyui mkoani Tabora.
Alisema kuwa kumekuwa na tabia ya baadhi ya viongozi hao wa vijiji kutokuwa waaminifu kwa kushindwa kusoma taarifa za mapato na matumizi kwa wananchi wao sanjari na na kukiuka Sheria za Fedha za umma na kanuni zao ambazo zimesababisha michango ya wananchi kutumika nje ya malengo kusudiwa.
“Wadiwani mnalo jukumu la kusimamia jambo hilo …niseme tu kwa watendaji watakao kiuka agizo hili watachukuliwa hatua za kisheria ili kulinda maslahi ya umma” alisema.
Alisema kila wananchi wanapochangia fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo na fedha ambazo zinakusanywa na vijiji kutokana na tozo mbalimbali zinazotokana na mapato yake ya ndani ni vema zikaandaliwa taarifa ya mapato na matumizi na kusomwa kwa wananchi ili kuondoa manunguniko juu ya fedha zao kufunjwa.
Dkt. Sengati alisema migogoro mingi ya kifedha katika vijiji imekuwa ikijotokeza kutokana na viongozi wao kutosoma mapato na matumizi.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka Madiwani kuhakikisha watendaji wa Vijiji wanasoma taarifa ya mapato na matumizi kila mwezi kwenye Kamati za Vitongoji na vijiji na baada ya hapo kila robo ya tatu wanazisoma kwa wananchi kupitia mkutano wa hadhara.
Wakati huo huo Dkt. Sengati amewapongeza wakazi wa wilaya ya Uyui kwa kuamua kuanzisha mashamba makubwa (block farm) ya koroshi katika Kijiji cha Karangasi.
Alisema hatua hiyo itasaidia kuleta mapinduzi makubwa ya kilimo na kuchochea ujenzi wa viwanda ambavyo vitasaisaidia wananchi kujikwamua kiuchumi.
Dkt. Sengati alitoa wito kwa maeneo mengine ya Mkoa wa Tabora kufungua mashamba makubwa ya maembe na mikorosho ili kuvutia wawekezaji katika viwanda.
Katika mkutano huo wajumbe wamemchagua Said Ntahondi kuwa Mwenyekiti na Shaban Katalambula kuwa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya yaUyui.