Meneja Mawasiliano wa TBL Plc, Amanda Walter,akizungumzia na wananchi wa Monduli wakati wa maadhimisho hayo
Mtaalamu wa masuala ya jinsia kutoka dawati la jinsia la Jeshi la Polisi, ASP Fatuma Mtambo akielimisha wananchi wa Kata ya Monduli wakati wa maadhimisho hayo.
Baadhi ya wadau wakiwa katika picha ya pamoja
Baadhi ya wadau wa kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia wakiwa na mabango yenye ujumbe wa kupunga vitendo hivyo.
***********************************
KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL Plc), mwishoni mwa wiki imeungana na wadau wengine wanaopinga vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo Serikali, kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto wilayani Monduli mkoa wa Arusha ambao vilevile mwaka huu imeshiriki kutoa elimu sehemu mbalimbali za nchi kupitia kampeni yake ya #Isiwe Sababu