Mkuu wa wilaya ya Songea, Mh. Polotet Mgema akizungumza na wananchi waliojitokeza kwa wingi kushuhudia makabidhiano ya gari kwa mshindi wa pili wa bahati nasibu ya promosheni ya Vodacom Shangwe Shangwena kutoka Songea, Mjasiriamali Gloria Kamanga mwishoni mwa wiki
Mkuu wa wilaya ya Songea, Polotet Mgema (wapili kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na mshindi wa promosheni ya Vodacom Shangwe Shangwena, Gloria Kamanga na familia yake, pamoja na Mkuu wa Mauzo Vodacom Kanda ya Nyanda za juu kusini, Macfadyne Minja (watatu kulia ) mara baada ya makabidhiano ya gari.
Mkuu wa wilaya ya Songea Mh.Polotet Mgema (kushoto ) akiwa amepozi na mshindi wa gari la promosheni ya Vodacom Shangwe Shangwena mkazi wa Songea, Gloria Kamanga na Mkuu wa Mauzo Vodacom Kanda ya Nyanda za juu Kusini, Macfadyne Minja.
Wakazi wa mjini Songea waliojitokeza stendi ya mabasi mjini humo kushuhudia makabidhiano ya gari aina ya Renault KWID kutoka Vodacom kwenda kwa mshindi wa bahati nasibu ya promosheni ya Vodacom Shangwe Shangwena, Gloria Kamanga (hayupo pichani ) mwishoni mwa wiki ambaye ni mjasiriamali mdogo katika soko la Manzese mjini Songea. Promosheni hiyo itawezesha watumiaji wa M-Pesa kujishindia magari mapya 5 pamoja na zawadi kemkem zenye thamani ya zaidi ya shilingi 3 bilioni, unachotakiwa kufanya ni kutumia huduma ya M-Pesa kadri uwezavyo katika msimu huu wa sikukuu.