Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Mhe.Dotto James akizungumza katika Mahafali Ya 44 Ya Taasisi Ya Ustawi Wa Jamii Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Mhe.Dotto James akimtunuku Cheti Mhitimu aliyefanya vizuri kwenye masomo yake.
*************************************
NA EMMANUEL MBATILO
Wahitimu wameaswa kuwa wazalendo, wawajibikaji na watu wenye maadili mema kwa jamii ya Tanzania na Taifa kwa ujumla kwani Mapinduzi ya kiuchumi yanategemea mapinduzi ya kifikra miongoni mwa wasomi.
Ameyasema hayo leo Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Mhe.Dotto James wakatia akiwatunuku vyeti wahitimu katika Mahafali Ya 44 Ya Taasisi Ya Ustawi Wa Jamii Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika Mahafali hayo Mhe.James amesema Serikali inatambua jinsi wataalam wa ustawi wa jamii walivyoweza kusaidia kuzuia matendo ya ukatili dhidi ya akina mama na watoto, kupunguza mimba na ndoa za utotoni, kuimarisha ustawi wa familia kwa kutoa unasihi na ushauri wa kitaalam, kuongoza mapambano dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya na kushiriki katika kupunguza maambukizi ya virusi vya ukimwi na unyanyapa katika jamii.
Aidha amesema hatua mlizochukua zitapunguza ama kuondoa kabisa pengo lililopo kati ya ubora wa wahitimu wanaozalishwa vyuoni na mahitaji ya soko la ajira.
Amesema kwa kutambua umuhimu wa rasilimali watu katika maendeleo ya nchi, Serikali ya Awamu ya Tano, iliamua kuwekeza kwenye elimu kwa kujenga miundombinu ya elimu, kutoa elimumsingi bila ada na kuongeza mikopo ya wanafunzi.
“Kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita ambapo kiwango cha uandikishaji wanafunzi na uwezo wa udahili umeongezeka katika ngazi zote”. Amesema Mhe. Dotto James.
Wanataaluma ya Maendeleo ya Jamii ni muhimu katika kuhamasisha, kuelimisha na kuwaongoza wananchi katika juhudi zao za kujiongezea kipato, kupunguza umasikini na kujiletea maendeleo kwa ujumla.
“Tumeona jinsi wataalam wa ustawi wa jamii walivyokuwa mstari wa mbele katika kusaidia kutambua na kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii”. Amesema Mhe.James.
Kwa upande wake Mhitimu wa Chuo hicho Bw.Moile loorbuluka amesema elimu waliyoipata inaweza kuwasaidia kwa kuanzisha biashara mbalimbali ambazo za kujitegemea sio kusubiri kuajiriwa.
“Ajira ipo ila ni nama wewe unavyojiweka kwenye soko kuweza kuajiriwa”. Amesema Bw.Loorbuluka.