Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo George Maiga aliyeshika mkasi akikata utepe rasmi kuashilia uzinduzi rasmi wa daraja jipya la wanafunzi wa awali katika shule ya msingi Goba Jijini Dar es Salaam ambalo limejengwa kwa ufadhili wa shirika la Ocode, kulia kwake ni mwakilishi wa mkurugenzi wa Ocode Digna Mushi akishuhudia tukia la uzinduzi huo.
Kaimu Mkurugenzi wa shirika la Ocode Digna Mushi alitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo kwa wadau mbali mbali wa sekta ya elimu na viongozi wa serikali ambao walihudhulia katika halfa ya makabidhiano ya darasa hilo pamoja na vifaa vingine vya elimu katika shule ya msingi Goba.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispa ya Ubungo George Maiga ambaye alikuwa mgeni rasmi katika halfa hiyo ya makabidhiano akizungumza jambo na wanafunzi pamoja na walimu wao ambao walifika katika hafla hiyo kwa ajili ya kuweza kushuhudia.
Baadhi ya wanafunzi wa awali wanaosoma katika shule ya msingi Goba wakiwa wamekalia moja ya madawati ambayo yametolewa na shirika la Ocode kwa lengo la kuwaondolea usumbufu wa kusoma katika hali ya mlundikano.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Goba Ambrose Mwakimbwala akizungumza na umati wa wadau wa elimu na viongozi wa serikali hawapo pichani wakati wa sherehe hizo za makabidhiano ya darasa moja, viti, madawati pamoja na meza za walimu.
Baadhi ya wafanyakazi wa shirika la Ocode wakiwa meza kuu wakifuatilia matukio mbali mbali amabyo yalikuwa yanaendelea katika halfa ya uzinduzi huo ambao ulifanyika katika viwanja vya shule hiyo ya Goba. Wadau mbali mbali wa maendeleo katika sekta ya elimu pamoja na viongozi wa serikali wakiwa wanasalimiana na kujadiliana mambo ya elimu jumuishi katika halfa hiyo ya makabidhiano ya darasa moja ambalo limejengwa kwa ufadhili wa shirika la Ocode.(PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU.
*************************************
VICTOR MASANGU, GOBA
Baadhi ya shule za awali na msingi zilizopo katika Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam zinakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo miundombivu chakavu ya madarasa, upungufu wa madawati,pamoja na matundu ya vyoo hivyo kupelekea wanafunzi kusoma katika mazingira ambayo sio rafiki na wengine kukaa chini na kwa mlindikano.
Katika kuliona hilo uongozi wa Shirika lisilokuwa la kiserikali la Organization for Community Development (OCODE) limeamua kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano katika kukabiliana na changamoto zilizipo kwa kuamua kutoa sapoti ya msaada wa madawati, meza pamoja na kuwajengea darasa moja la elimu ya awali katika shule ya msingi goba ili kuondokana na usmbufu wanaoupata wanafunzi hao.
Akizungumza katika halfa ya kukabidhi madawati na darasa hilo Mwakilishi kutoka Shirika la Ocode Digna Mushi ambaye alimwakilisha mkurugenzi mtendaji alibainisha kwamba kwa sasa wanatekeleza mradi katika shule za msingi nne zilizopo katika manispaa ya Ubungo na kwamba lengo kubwa ni kuwasaidai wanafunzi waweze kupata elimu ambayo ni jumuishi.
“Leo tupo hapa kama shirika la Ocoede na mimi nipo kwa niaba ya Mkirugenzi mtendaji tunatekeleza mradi huu kwa shule mbali mbali na leo tunakabidhi darasa moja mbalo limeshakamilika ambalo limejengwa maalumu kwa ajili ya wanafunzi wa awali katika shule hii ya msingi,goba pia tumetoa na madawati,pamoja na meze za walimu hii yote ni kuhakikisha kwamba tunaboresha sekta ya elimu katika shule zetu za awali na msingi,” alisema Mushi.
Aidha Kaimu huyo Mkurugenzi alibainisha kuwa kama shirika wameshatoa misaada mbali mbali katika shule za msingi ikiwemo kuwasaidia katika ujenzi wa miundombinu ya madarasa pamoja na kuwapatia madaati, pamoja na meza kwa ajili ya walimu ili kuweza kufikia malengo ambayo wamejiwekea ya kuwasaidia watoto wa lika mbali mbali ikiwemo walemavu.
Kadhalika alifafanua kwamba katika utafiti ambao tayari wameshaufanya katika baaadhi ya shule zilizopo katika masispaa ya ubungo wameweza kubaini kuwepo kwa watoto 62 ambao wana mahitaji maalumu na kwamba tayari baadhi yao wameshapatiwa msaada katika awamu ya kwanza na wengine wataendelea kupatiwa sapoti kulingana na mahitaji yao husika ikiwemo kuwapatia vifaa maalumu.
“katika shule hii ya msingi Goba sisi kama shirika tulibaini kuwepo kwa changamoto mbali mbali hivyo kwa kuanzia tumeona tutoa mchango wetu kwa kuwajengea darasa moja watoto awali, madawati, viti, pamoja na meza bila kusahau vifaa mbali mbali amabvyo vitatumika kwa ajili ya kuwafundishia wanafunzi waweze kuelewa vizuri pindi wanapokuwa darasani,”alisisitiza.
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Goba Ambrose Mwakimwala ametoa pongezi zake za dhati kwa shirika la Ocode kwa msaada huo wa kuwajengea darasa na kuwapatia madawati ambayo yatakuwa ni mkombozi mkubwa zaidi katika kuwasaidia wanafunzi kuondokana na changamoto ya kukaa chini na wengine kusoma wakiwa katika hali ya mlundikano.
“Kwa kweli nipende kutoa shukrani zangu mimi kama mwalimu Mkuu kwa shirika hili la Ocode kwa kutupatia msaada huu ambao utaweza kuleta matokeo chanya kwa wanafunzi wetu ambao hapo aawali walikuwa wanakabiliwa na changamoto katika suala zima la kukaa chini hivyo nina imani kwa kuanzia hatua hii itaweza kuwafanya wasome katika mazingira ambayo ni rafiki.
Naye Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo George Maiga ambaye alikuwa mgeni rasmi katika halfa hiyo alibainisha kwamba shirika la Ocode limeweza kuwa mstari wa mbele katika kusaidia kwa hali na mali kuboresha sekta ya elimu hivyo watakuwa tayari kushirikiana bega kwa bega katika kuzitatua changamoto za wanafunzi zinazowakabili hasa katika miundombinu ya madarasa.
Nao baadhi ya wazazi na walezi ambao walifika katika halfa hiyo ya makabidhiano walisema kwamba wana imani kubwa na shirika hilo la Ocode kwa kuweza kuwawezesha vifaa mbali mbali vya kuwafundishia watoto wao na kwamba kutaweza kupunguza kwa kiasi Fulani changamoto ya kusoma wakiwa katika hali ya mlundikano madarasani.
Shirika lisilokuwa la kiserikali la Ocode limekuwa likiendesha miradi yake mbali mbali katika Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es Salaa ikiwemo mkradi ya elimu ambayo imeweza kuzigusa shule nne zilizopo katika kata mbali mbali lengo ikiwa ni kutoa elimu jumuishi ikiwa sambamba na kuwajengea madarasa, pamoja na kuwapatia madawati, viti na meza ili kuboresha sekta ya elimu.