************************************
Na Goodluck Sendula, Manyara;
Habari za wakati huu Mwandishi na Mwanabloga?
Natanguliza shukrani kwa nafasi yako ya kufungua makala hii yenye manufaa wakati huu wa mapambano dhidi ya COVID 19 duniani. Niwakumbushe tu kuwa Dawa haimtibu Mgonjwa bali Imani juu ya Dawa ndiyo Tiba thabiti kwa Mgonjwa.
Mwaka 2020 umekuwa wa kihistoria kwa nchi ya Tanzania na Dunia kwa ujumla kutokana na Vimbwanga vyake.
Kwa upande wa Tanzania, mwaka 2020 umefungamana na Imani ya Mungu inayoendeleza kushangaza Mataifa na kuzidi kujiuliza, Kwani Imani ni nini? Imani inaweza kuwa na maana ya Uhakika wa Mambo yasiyoonekana yanayotarajiwa bila uwezekano wa kibinadamu.
Mungu hawezi kuonekana dhahiri kwa macho isipokuwa Matendo yake yanaonekana wazi pale akili za kibinadamu zinapogonga mwamba.
Uchomozi wa mwaka 2020 ni kupitia Ugonjwa wa COVID 19 ambao uliibuka miisho ya 2019 nchini China na kusambaa Duniani kote kwa njia ya ‘hewa nyevu’ katika mianzo ya 2020 mpaka sasa.
Takwimu za Ugonjwa huu zimeufanya uingie katika rekodi ya Magonjwa ya milipuko kwani watu zaidi ya 1,000,000 (Milioni) wamethibitishwa kufa huku waambukizwa wakizidi 35,000,000 (Milioni 35) duniani ndani ya miezi michache tu (https://covid19.who.int/?)
Wakati Dunia iking’ang’ana kunawa mikono, kutokusalimiana kwa mikono, Kuvaa Barakoa, Kukaa umbali wa mita moja toka mtu hadi mtu, kujitenga na kujifungia ndani, kusiriba maporomoko ya Uchumi; Hali imekuwa tofauti sana kwa nchi ya Tanzania kwani: