**********************************
NA DENIS MLOWE, IRINGA
MKUU wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela amelisisitiza Baraza la madiwani kuhakikisha wanakamilisha madarasa 27 yanayohitajika kwa ajili ya wanafunzi wanaotarajia kuanza kidato Cha kwanza januari 2021.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao Cha kwanza Cha Baraza la madiwani Manispaa ya Iringa tangu kumalizika uchaguzi mkuu na kuapa rasmi, Kasesela alisema kuwa kutokana na matokeo ya mitihani darasa la Saba Wana wanafunzi 1323 ambao hawana sehemu za kusomea pindi shule zikifunguliwa januari.
Hivyo kutokana na Hilo Kasesela alitoa wito kwa Baraza la madiwani kuanza na mjadala huo kuhakikisha ndani ya wiki tatu madarasa 27 yawe yamekamilika wanafunzi wanaanza masomo pindi ifikapo Muda huo.
Alisema kuwa halmashauri Pekee yenye idadi ya wanafunzi wengi waliochaguliwa kujiunga na kidato Cha kwanza Manispaa hivyo madiwani Mara baada ya kuapishwa jukumu la kwanza ni kuhakikisha madarasa hayo yanapatikana.
Aidha aliwataka madiwani hao kuhakikisha Manispaa ya Iringa inaendelea kudumisha suala la usafi ambapo Manispaa imekuwa katika tano Bora kila mwaka.
Aliongea kuwa atahakikisha kwamba anashirikiana kwa hali na mali na madiwani wote waliochaguliwa katika baraza jipya lengo ikiwa na kuwataka kusikiliza kero za wananchi ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi na kuleta maendeleo chanya ya kimaendeleo.
Alisema kuwa Baraza la Sasa lilloko na chama Cha Mapinduzi kina madiwani ambao wachapakazi na kuwataka kufanya kazi kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo ambayo walikuwa wakitaka hivyo kila mmoja hakikishe wanatekeleza ilani.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Ahmid Njovu alisema kwamba madiwani wote ambao wameapishwa kwa mujibu wa taratibu na sheria wataanza mara moja kutekeleza majukumu yao ya kuwatumikia wananchi katika maeneo yao mbali mbali ikiwemo kusikiliza changamotona kuzitafutia ufumbuzi.
Alisema kuwa atahakikisha wanatatua changamoto mbalimbali za wananchi na kukamilisha miradi ya naendeleo ambayo imekwisha Anza katika kata mbalimbali.
Naye Meya wa Manispaa ya Iringa, Ibrahim Ngwada aliwaondoa hofu watumishi wa Manispaa ya Iringa na kuwataka kufanya kazi kwa weledi mkubwa na kuwaomba ushirikiano katika kutatua changamoto za wananchi.
Alisema kuwa atahakikisha wanashirikiana na madiwani wote katika kutatua kero zao ili Manispaa isonge mbele kwa Kasi zaidi.
Aidha aliwataka madiwani wasiwe watu wa kukubaliana na kila Jambo katika Baraza na kuwapa wito kwamba penye kukosoa wakosoe ,penye kusifia wasifie Bila hofu yoyote.