Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. William Tate Olenasha, ameapa kiapo cha Utii cha Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki
Mhe. Olenasha ameapa kiapo hicho na kushuhudiwa na Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Martin Ngoga pamoja na wabunge wengine wanaounda Bunge hilo ili kumwezesha kushiriki kwenye Bunge hilo kama Naibu Waziri anayeshughulikia masuala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mhe. Olenasha ameapa kiapo hicho akiwa katika Ofisi za Wizara zilizopo kwenye Mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma wakati wa kikao kilichofanyika kwa njia ya mtandao tarehe 10 Desemba 2020.
Aidha, kikao hicho kimehudhuriwa na Wabunge wa Bunge hilo ambao wengi wameshiriki kutokea kwenye nchi zao wakati Mhe. Spika akiwa Makao Makuu ya Bunge hilo jijini Arusha.
Kikao hicho, pamoja na mambo mengine kimejadili Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge la Afrika Mashariki ya Masuala Mtambuka
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. William Tate Olenasha akiapa kiapo cha utii na uadilifu mbele ya Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Ngoga Martin. Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. William Tate Olenasha akiapa kiapo cha utii na uadilifu mbele ya Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Ngoga Martin
Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Tanzania, Mhe. Josephine Sebastian Lemoyan akimtambulisha Mhe. Olenasha kwenye Bunge hilo kama Mjumbe mpya Mhe. Olenasha akisaini Hati ya Kiapo baada ya kula kiapo cha utaii cha kushiriki Bunge la Afrika Mashariki