Moja ya mkurugenzi wa kampuni ya Asas Fesail Abri akitoa moja ya msaada .
Moja ya risiti ambazo zinaonyesha msaada wa elfu kumi ya mwaka 1981 ikiwa mchango kwa ajili ya michezo
*********************************
NA DENIS MLOWE, IRINGA
KATIBU wa Chama Cha Soka Mkoa wa Iringa,(IRFA) Dk. Ally Ngallah ameipongeza kampuni mama ya ASAS inayojishughulisha na uzalishaji wa maziwa Bora nchini ya Asas kwa kuwa mfano Bora katika kuchangia na kukuza michezo nchini.
Akizungumza na wanahabari,DK.Ngallah alisema kuwa kampuni ya ASAS hawakuanza jana wala juzi kuchangia michezo hali ambayo wengi wanadhani kwamba imejitokeza miaka ya hivi karibuni katika kuchangia michezo.
Alisema kuwa kutokana na kampuni hiyo kujidadavua kuwa moja ya kampuni kubwa nchini kusaidia Michezo ndio maana mmoja ya wakurugenzi wake Feisal Abri kuchaguliwa kwenye kamati ya kusaidia Stars Ishinde.
Alisema kuwa wameanza kuchangia michezo mbalimbali miaka ambayo vijana wengi hawajazaliwa Hali ambayo inastaajabisha kwa kiasi kikubwa.
“Tuna jambo la kujivunia kwetu viongozi wa Mpira na Vilabu ambao tunafaidika na Misaada yao mpaka leo kwani imekuza sana soka na michezo mingine nchini.”alisema
Alisema kuwa Kuna risiti ambayo imeonyesha ni miaka mingi iliyopita wakichangia mchezo wa soka Hali ambayo ni Jambo la kupongeza na kuifanya kampuni hiyo kujitofautisha na kampuni nyingine katika kusaidia jamii ya michezo.
Alisema kuwa licha ya kutoa misaada tangu kuanzishwa kwake kampuni hiyo inadhamini michezo mbali mbali ikiwemo ligi soka daraja la tatu mkoa wa Iringa, Mashindano ya Ndondo Cup yanayofanyika jijini dar es Salaam,
Kuidhamini timu ya Lipuli na kutoa michango nje ya udhamini unaofanywa na mkurugenzi wake Salim Abri katika kusaidia Lipuli na timu nyingine mkoani hapa.
Aliongeza licha ya kuchangia michezo kampuni hiyo imekuwa msaada mkubwa kwa jamii Hali ambayo inatakiwa kuigwa na wadau wa maendeleo nchini.
Alitoa wito kwa watanzania kuendelea kuzipenda bidhaa za Asas Dairies Ltd kutokana na kuendelea kuongoza katika ubora na kuwa lengo la kampuni hiyo ni kuona ubora huo unaendelea zaidi na kila mwaka kuendelea kufanya vema na kuifanya serikali kukusanya Kodi kutokana na bidhaa zinazozalishwa.
Pia alipongeza watanzania na watumiaji wa bidhaa za Asas Dairies Ltd kutokana na ushirikiano mkubwa wanaoutoa kwa kuendelea kutumia maziwa yanayozalishwa na kampuni hiyo ya Asas Dairies Ltd Iringa hali ambayo inasaidia kampuni hiyo kuendelea kudhamini michezo nchini.
Dk. Ngallah alisema kuwa Niaba ya IRFA Tunawashukuru sana uongozi wa kampuni ya Asas na Mungu awazidishie kwani licha ya kulipa Kodi mbalimbali kubwa tangu miaka hiyo wamekuwa hasiti kuchangia michezo na jamii ya mkoa wa Iringa.