***********************************
Makamo wa kwanza wa Rais wa Serikali ya mapinduzi Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amesema Serikali ya Umoja wa Kitaifa si kambi ya wanasiasa kupeana nyadhifa navyeo bali ni chombo cha matarajio kwa wazanzibari
Pia amesema kimeundwa kwa minajili ya kuyafikia maridhiano ya kweli ,kuendeleza umoja na mapatano yatakayoondoa chuki,hasama na mgawanyiko .
Amesema serikali ya umoja wa kitaifa pekee haitaondosha kasoro kwa katiba na sheria bali kinachotakiwa ni kupatikana kwa muafaka wa kijamii utakaozika hasama, visasi, chuki.
Pia amesema kuna haja ya kuondosha hali kutoamimiana miongoni mwa viongozi ili kuwaweka pamoja na kuwaanisha wanachi wa zanzibar.
Amesema ipo haja ya makusudi ya kuondokana na taaswira hasi ya kuachana na mifarakano badala yake wananchi waishi kwa mapatano na umoja.
Makamo huyo wa Kwanza wa Rais amesema ipo haja ya kubaini ni kwanini kila unapofanyika uchaguzi na kumalizika huacha athari aidha za watu kulalamika ,kususia au kugawanyika .
Amesema ni jukumu la msingi kwa serikali iliopo madarakani la kuwafanya watu waishi bila kuwekeana mifundo kwenye mioyo yao.
Kwa muktadha huo Maalim seif amesema Act wazalendo kitashirikiana na serikali ya awamu ya nane chini ya Rais Dk Mwinyi kwa matarajio ya kusonga mbele.
Amesema wataendeleza ushirikiano kwa lengo la kuwaweka pamoja wazanzibari , wapendane , washirikiane na kufanya kazi kwa kuaminiana.
Hata hivyo amesema SUK ni chombo cha kusafiria na ili msafiri afike salama mahali anakokwenda njia pekee ni viongozi kuaminiana na wananchi wakoshirikiana .