Na
Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Shirika
la World Vision limetoa msaada wa vifaa tiba na vifaa vya kuanzishia huduma ya
Tiba Mtandao vyenye thamani ya Shilingi Milioni 148.8 ili kukinga magonjwa ya
kuambukiza na kusaidia matibabu katika vituo vya kutolea huduma za afya mkoani
Shinyanga.
Vifaa
hivyo vimekabidhiwa leo Jumanne Disemba 8,2020 na Mratibu wa Mradi wa ENRICH
unaotekelezwa na Shirika la World Vision, Dk. Frank Mtimbwa kwa Katibu Tawala
Mkoa wa Shinyanga ndugu Albert Msovela wakati wa kikao cha kutathmini maendeleo
ya Mradi wa ENRICH kilichofanyika katika ukumbi wa Karena Hoteli Mjini
Shinyanga.
Mratibu
wa Mradi wa ENRICH unaotekelezwa na Shirika la World Vision kwa Ufadhili wa
Serikali ya Canada Dk. Frank Mtimbwa amesema vifaa hivyo vyenye thamani ya
shilingi 148,816,000/= vitagawiwa katika halmashauri zote sita za mkoa wa
Shinyanga ambazo ni Kahama Mji, Msalala, Ushetu,Shinyanga, Manispaa ya
Shinyanga na Kishapu.
Amevitaja
vifaa hivyo kuwa ni Smart Tv ,Oxygen Cylinder,Nebulizer compreser, Nebulizer
Mashine, Suction mashine leg operator, Suction mashine heavy duty, Pulse
Oximeter, Oxygen nasal catheter, Mashine za kupimia msukumo wa damu mwilini (BP
Machine) na Infra –led thermometer.
Vifaa
vingine ni mifuko ya kuhifadhia taka hatarishi (Biohazards bags), Dawa maalumu za
kutakasia (Disinfectants) zenye ujazo wa lit 5 kila moja, vikinga uso wakati wa
kumuhudumia mgonjwa (Protective face shields na Eye Protective googles), P/50
surgical gloves, Examination gloves, Barakoa tiba (surgical masks), hand washing
soap, Hand washing system 100Lts na Hand washing system 50Lts.
Amesema
vifaa hivyo kupitia mradi wa ENRICH unaolenga kuboresha lishe ya mama na mtoto
unaotekelezwa katika halmashauri tatu za wilaya kati ya 6 za mkoa wa Shinyanga
ambazo ni Kishapu, Shinyanga na Kahama Mji.
“Tunapofikia mwisho wa huu mradi tumeangalia changamoto
zinazotukabili tumeona leo tukabidhi vifaa hivi kwa ajili ya kuokoa maisha
katika halmashauri zote za wilaya mkoani Shinyanga”, amesema Dk. Mtimbwa.
“Pia mradi umefanya tathimini kwa kushirikiana na Wizara ya OR
TAMISEMI, Wizara ya Afya, Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa na Halmashauri kwa ajili
ya kuanzisha huduma ya Tiba Mtandao ili kupunguza changamoto zinazowakabili
watoa huduma wa afya katika vituo vya kutolea huduma za afya ambavyo vina
changamoto ya watumishi.
Hivyo tunahitaji wawe wanapata ushauri wa Kibingwa
kabla ya kumpeleka mgonjwa sehemu nyingine ili kupata matibabu zaidi. Kwa maana
hiyo kuna baadhi ya vituo vya vitafungwa mfumo wa Tiba Mtandao hasa zile za
ngazi ya chini kabisa ya rufaa ambavyo tutavikabidhi Runinga”,ameongeza.
Akipokea
vifaa hivyo, Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela amelishukuru
Shirika la World Vision kwa msaada huo wa vifaa tiba vya kisasa ili kuwezesha
vituo vya afya kutoa huduma za kisasa zaidi.
“Serikali ya mkoa wa Shinyanga tunawashukuru World Vision kwa
msaada huu mkubwa kwa sababu sasa vituo vyetu vya afya japo siyo vyote tunaenda
kupunguza changamoto zilizopo. Nina imani watalaamu wetu wa afya watatumia
vifaa hivi kuboresha huduma za afya na kutumia vifaa hivi kwa malengo
yaliyokusudiwa na tunaahidi kuendelea kushirikiana nanyi katika kuboresha
huduma za afya”,ameongeza
Msovela.
Kwa
upande wake, Mganga Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dk. Yudas Ndungile amesema vifaa
hivyo vitasaidia katika masuala ya lishe na kuokoa akina mama wajawazito hasa
wanapokuwa katika eneo la Upasuaji na mfumo wa mawasiliano katika kuhakikisha
huduma ya upasuaji kwa njia ya mtandao au ushauri kwa njia ya mtandao
vitafungwa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.