Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Mhe. Jaji mstaafu Mathew Mwaimu (katikati) pamoja na Makamu wake, Mhe. Mohamed Khamis Hamad (wa pili kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa kikao cha kujadili taarifa ya Tume ya ukaguzi wa magereza na vituo vya polisi. Wengine kutoka kushoto (waliokaa) ni: Mwakilishi wa Inspekta Jenerali wa Polisi, DCP Fredenand Mtui, Mwakilishi wa Ofisi ya Msajili Mkuu Mahakama ya Rufani, Mhe. Silvia Lushasi na Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Wizara ya Katiba na Sheria, Bw. Burton Mwasomola. Kikao hicho cha siku moja kimefanyika ukumbi wa mikutano ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma leo Desemba 8, 2020.
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Mhe. Mohamed Khamis Hamad akiwasilisha taarifa ya ukaguzi ya magereza na vituo vya polisi kwa wadau wakati wa kikao hicho cha siku moja.
Mwakilishi wa Kamishna Jenerali wa Magereza, ACP Isaack Kangura akichangia hoja wakati wa majadiliano ya taarifa hiyo.
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mhe. Mathew Mwaimu (Jaji mst.) akisisitiza jambo wakati wa majadiliano ya taarifa hiyo ya ukaguzi.
Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bi. Fatuma Muya akichangia hoja wakati wa kikao hicho cha siku moja.
Mwenyekiti wa THBUB, Mhe. Mathew Mwaimu (Jaji mst.) akiwashukuru washiriki wa kikao muda mfupi kabla ya kufunga kikao hicho.
Baadhi ya washiriki wa kikao cha siku moja cha kujadili taarifa ya THBUB ya ukaguzi wa magereza na vituo vya polisi wakifuatilia mjadala.