Akimwakilisha katibu mkuu wa sekta ya uchukuzi Mhandisi Aron Kisaka akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa wadau wa sekta ya madini kuhusu umuhimu wa huduma za hali ya hewa iliyofanyika jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA) Dk. Agnes Kijazi,akizungumza kwenye Mkutano wa wadau wa sekta ya madini kuhusu umuhimu wa huduma za hali ya hewa iliyofanyika jijini Dodoma.
Mtendaji Mkuu wa Wachimbaji Madini Tanzania na Kamishana Tume ya Madini Haroun Kinega,akizungumza katika Mkutano wa wadau wa sekta ya madini kuhusu umuhimu wa huduma za hali ya hewa iliyofanyika jijini Dodoma.
Muwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Bw.Robert Sunday akitoa neno la shukrani kwenye Mkutano wa wadau wa sekta ya madini kuhusu umuhimu wa huduma za hali ya hewa iliyofanyika jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa wadau wa sekta ya madini kuhusu umuhimu wa huduma za hali ya hewa iliyofanyika jijini Dodoma.
Akimwakilisha katibu mkuu wa sekta ya uchukuzi Mhandisi Aron Kisaka akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua Mkutano wa wadau wa sekta ya madini kuhusu umuhimu wa huduma za hali ya hewa iliyofanyika jijini Dodoma.
…………………………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
Kutolewa kwa taarifa sahihi za hali ya hewa kwa wachimbaji wa madini kwa wakati kunatajwa kuwa kutasaidia kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa na kupunguza madhara yatokanayo mabadiliko ya hali ya hewa.
Hayo yamebainishwa Jijini Dodoma na Mhandisi Aron Kisaka wakati akimwakilisha katibu mkuu wa sekta ya uchukuzi wakati akifungua mkutano wa wadau wa sekta ya madini kuhusu umuhimu wa huduma za hali ya hewa.
Mhandis Kisaka amesema kuwa taarifa hizo zitazisaidia mamlaka zinazohusika kupanga mipango ya kukabiliana na majanga ndani ya sekta yatokanayo na hali mbaya yahewa kama maporomoko ya udongo.
“Katika mkutano huu washiriki watapata fursa ya kufahamu faida za utumiaji wa taarifa za hali ya hewa kwa sekta ya madini ili kupunguza maafa yatokanayo na hali ya hewa” amesema Mhandisi Kisaka.
Amesema kuwa matumizi ya huduma za hali ya hewa yanatarajiwa kuongeza tija,ufanisi na usalama katika shughuli zinazohusianana utafutaji,uchimbaji madini na uendeshaji wa migodi.
“Lengo la mkutano huu ni kujenga uelewa wa pamoja kwa wadau wa sekta ya madini juu ya sheria na.2 ya mamlaka ya hali ya hewa Tanzania,ikiwemo pamoja na upatikanaji wa mahitaji mahususi ya wadau wa sekta ya madini hususan wachimbaji wadogo wadogo ili kuimarisha usalama wao migodini” amesema.
Aidha Mhandisi Kisaka amewakumbusha umuhimu wa matumizi ya taarifa sahihi za hali ya hewa kwa maendeleo ya shughuli mbalimbali.
“TMA inawataalam bobezi wa kutosha hivyo tuitumie taasisi yenu kwa matokeo chanya ikiwa ni pamopja na kupata eimu au mafunzo ya kuelewa zaidi sayansi ya hali ya hewa” amesema.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA) Dk. Agnes Kijazi amesema kuwa mamlaka ya hali ya hewa inawajibu wa kutoa huduma mahususi kwaajili ya sekta mbalimbali nchini ikiwemo ya madini.
“Ni matarajio yetu kuwa wadau watapatiwa elimu ya matumizi sahihi ya huduma za hali ya hewa na huduma zitakazo patikana endapo watazitumia vyema taarifa hizo” amesema Dkt Agnes Kijazi.
Aidha Dkt.Kijazi ambaye pia ni Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) amesema kuwa wanatarajia matokeo chanya ya warsha kwa kuongezeka matumizi ya taarif zahali ya hewa na hivyo kusaidia kupunguza majanga yatokanayo na hali mbaya ya hewa kwa sekta ya madini hususani wachimbaji wa madini.
Akimwakilisha Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa mamlaka ya hali ya hewa Tanzania Robert Sunday amesema kuwa madhumuni ya mkutano wa sekta ya madini na mamlaka ya hali ya hewa ni kuunganisha nguvu katika kuhakikisha kunaongeza pato la taifa na usalama wa watu na mali zao.