Waziri mteule wa Viwanda na Biashara Mhe.Geoffrey Mwambe akipata maelezo kutoka kwa Meneja Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma Wakala wa Vipimo (WMA)., Bi.Irene John alipotembelea banda la WMA katika Maonesho ya Tano ya bidhaa za Viwanda yanayofanyika katika Viwanja Maonesho vya Mwl. Nyerere (Sabasaba) Jijini Dar es Salaam.
***************************
Waziri mteule wa Viwanda na Biashara Mhe.Geoffrey Mwambe afurahishwa na huduma zinazotolewa na Wakala wa Vipimo (WMA) katika Maonesho ya Tano ya Bidhaa za Viwanda yanayoendelea katika Viwanja Maonesho vya Mwl. Nyerere (Sabasaba) Jijini Dar es Salaam.
WMA imekua ikitoa elimu juu ya matumizi sahihi ya vipimo kwa wateja ambao wamekuwa wakifika katika banda lao kwenye maonesho ya Bidhaa za Viwanda.