Maofisa wa TAKUKURU Wilayani Kiteto Mkoani Manyara, wakitoa elimu kwa wananchi wa Kiteto, juu ya mapambano ya kuondokana na matukio ya rushwa.
Wananchi wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, wakipatiwa elimu ya kupiga vita rushwa kutoka kwa maofisa wa TAKUKURU Wilayani Kiteto waliokuwa kwenye uelimishaji wa matukio ya rushwa.
***********************************
Na Mwandishi wetu, Kiteto
OFIS ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilayani Kiteto Mkoani Manyara, imeendelea na majukumu yake jana na leo 06.12.2020 kwa kutekeleza majukumu ya uelimishaji.
Mkuu wa TAKUKURU Mkoani Manyara, Holle Joseph Makungu amesema lengo ni watumishi hao kuendelea kutoa elimu kwa jamii na kuhakikisha wanapambana ili kuondokana na vitendo vya rushwa.
“Tukishirikiana kwa dhati kupiga vita dhuluma za aina zote, haki itatamalaki Manyara na pia jukumu la kupambana na rushwa liwe la kula mmoja wetu,” amesema Makungu.
Amesema wapambanaji hao wa Wilaya ya Kiteto, Emmanuel Manyutwa akisaidiana na Burton Chidodolo, jana katika ukumbi wa shule ya sekondari ya Lesoit walitoa elimu ya rushwa kwa wajumbe wa kamati ya usimamizi wa Msitu wa Jamii (Suledo).
Amesema leo Desemba 6 wanaendelea na kufanya onesho katika mnada wa Kata ya Sunya.