Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akizungumza na Wasanii wa Sanaa za Ufundi (hawapo pichani) kuhusu azma ya serikali ya kuendeleza sekta ya sanaa hivyo watoe maoni ya mambo gani yaboreshwe kuendeleza tasnia hiyo, leo Desemba 04, 2020 Jijini Dar es Salaam, kufuatia tamko la Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli la kuendeleza Sanaa alipokuwa akifungua bunge.
Mwakilishi wa Kikundi cha Wanawake wanaofanya Sanaa ya Uchoraji Safina Kipokota (kushoto) akimkabidhi zawadi Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi,leo Desemba 04,2020, Jijini Dar es Salaam, katika kikao na wadau wa Sanaa za Ufundi kujadili namna ya kuendeleza tasnia ya hiyo kufuatia tamko la Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli la kuendeleza Sanaa alipokuwa akifungua bunge.
Msanii wa Ubunifu wa Mavazi Khadija Mwanamboka akitoa ombi kwa serikali kuzungumza na makampuni binafsi kuchangia katika Mfuko wa Sanaa na wasanii wawasaidie kutangaza bidhaa zao,Leo Desemba 04,2020 Jijini Dar es Salaam, katika kikao cha wadau wa sanaa za ufundi cha kujadili mikakati ya kuendeleza tasnia ya filamu kufuatia tamko la Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli la kuendeleza Sanaa wakati alipokuwa akifungua bunge.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi (aliyeketi watatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wasanii wa Sanaa za Ufundi waliyohudhuria kikao cha kujadili mikakati ya kuendeleza tasnia hiyo leo Desemba 04, 2020 Jijini Dar es Salaam mara baada ya kumalizika kikao hicho.
Msanii wa Uchoraji wa Katuni Nathan Mpangala akitoa ombi kwa serikali kuangalia suala la gharama za kusajili youtube channel kwani baadhi yao hutumia akaunti hizo kutafuta masoko ya kazi zao na siyo kuhabarisha umma, Leo Desemba 04,2020 Jijini Dar es Salaam, katika kikao cha wadau wa sanaa za ufundi cha kujadili mikakati ya kuendeleza tasnia hiyo kufuatia tamko la Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akifungua bunge. Msanii wa Ubunifu wa Mavazi Merinyo Ndesumbuka akitoa ombi kwa serikali kushauri katika masuala mbalimbali ya uendeshaji wa shuguli za sanaa ,Leo Desemba 04,2020 Jijini Dar es Salaam, katika kikao cha wadau wa sanaa za ufundi cha kujadili mikakati ya kuendeleza tasnia ya filamu kufuatia tamko la Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli la kuendeleza Sanaa kilichofanyika jijini Dar es Salaam kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
***********************************
Anitha Jonas – WHUSM, Dar es Salaam
05/12/2020
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbasi amesema kuanzia mwaka 2021 kutakuwa Maonesho ya Kitaifa ya Sanaa za Ufundi nchini.
Dkt. Abbasi ametoa kauli hiyo leo Desemba 04, Jijini Dar es Salaam, katika mkutano na Wasanii wa Sanaa za Ufundi ikiwa ni mwendelezo wa vikao vyake vya kukutana na makundi mbalimbali ya wadau wa Sanaa kwa lengo la kujadili namna ya kukuza na kuendeleza sekta ya Sanaa kwa kuzingatia ahadi ya Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli katika hotuba yake wakati akifungua Bunge.
Akizungumza katika kikao hicho Dkt.Abbasi alisisitiza kuwa serikali imedhamiria kusaidia sekta ya sanaa, kwa kukuza masoko na kujenga mazingira rafiki ya kuendeleza sanaa nchini.
“Viongozi wa Mashirikisho na vyama nendeni mkafanye utafiti wa Maonesho ya kazi za Sanaa za Ufundi Kimataifa na mnilete kalenda inayoonyesha matukio hayo, na nchi inayoandaa maonesho hayo ili tuwasiliane na balozi zetu kuona namna tunaweza kuwasaidia, sisi pia kama wizara kila patakapo kuwa na matukio makubwa au mechi kubwa pale Uwanja wa Benjamin Mkapa nitatoa eneo kwa wasanii wa Sanaa za Ufundi kuonyesha na kuuza kazi zao,”alisema Dkt.Abbasi.
Akizungumza katika kikao hicho Dkt.Abbasi alisisitiza wasanii kutumia vyama vyao na Mashirikisho kutoa maoni ya mambo wanayokwamisha uendeshaji wa kazi zao ikiwemo utitiri wa kodi na tozo ambazo nikubwa zinazokwamisha shughuli hizo.
Naye Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa Taifa Godfrey Mngereza ahidi kupokea maoni yote ya wadau hao na kusema atayafanyia kazi ikiwemo kuandaa mpango wa kutoa mafunzo kwa wasanii wa Sanaa za Ufundi ya namna ya kufanya biashara katika mfumo wa kisasa kwa kuweka kipao mbele thamani ya kazi zao.
Halikadhalika nae Msanii wa Sanaa ya Uchoraji Hasmain Raza alitoa ombi kwa Serikali la kuangalia muundo wa majukumu kwa taasisi ya BASATA katika uendeshaji, kwa kuomba ianzishe Idara au Vitengo cha Muziki kwa kila sanaa wanayoisimamia, badala ya sasa hali ilivyo sasa vitu vyote kuendeshwa kwa pamoja.