Kushoto jaji mstaafu Dkt Fauz Twaib akizindua moja ya chapisho kwa ajili ya kusaidia wanasheria msaada wa kisheria kulia ni Rais wa Chama Cha mawakiliTanganyika (TLS)Dkt Nshala Rugemela
Jaji mstaafu Dkt Fauz Twaib akiongea na vyombo vya habari mara baada ya kufungua mkutano huo
…………………………………………………………………………………………
Na Woinde Shizza ,ARUSHA
CHAMA Cha mawakili Tanganyika (TLS) kimewakutanisha wanataaluma wa anuai (professional diversity )800 kujadili maswala mbalimbali wanayokumbana nayo ,kujua fursa ,changamoto zilizopo katika taaluma zao haswa kwa upande wa Sheria .
Akiongea katika mkutano wa kwanza wa anuai za kitaaluma ulioandaliwa na Chama hicho uliofanyika mkoani Arusha Jana Rais wa Chama hicho Dkt.Nshala Rugemeleza alisema kuwa wamekutana kujua fursa zilizopo katika kila taaluma ,kuangalia ni jinsi gani wanasheria wanaweza kushirikiana na watu wa taaluma mbalimbali nakuweza kufanya shughuli zao kwa ufanisi mkubwa zaidi pamoja na kupanua wigo wa shughuli zao ili kuweza kwa pamoja kuwedadisi fursa zilizopo.
Alisema kuwa sheria huwezi kufanya peke yako Kama sheria ilivyo ni vyema ukajua watu wa kada mbalimbali wanafanya kitu gani , maana sheria za nchi yetu zinagusa kada zote na fani zote lakini mwisho wa siku nijukumu la mwanasheria kutoa tafsiri ya hizo sheria
“Bunge limeweza kutunga sheria ambazo zinagusa karibu fani zote lakini mwisho wa siku mwanasheria ndio anatakiwa atowe mwongozo wa hizo sheria kwa kila kada,Ila watu wa kada hizi wamekuwa wakitaka kutoa tafsiri zao ni vyema watu wakaweza kukutana na kujadili namna gani wanaweza kashirikiana na wanasheria ,wasanifu wa majengo ,wanahabari ,wahasibu ili kujenga ushirikiano na kuweza kukuza fursa na kutumia teknolojia za kisasa kuweza kukuza uwanda wa ufanyaji wa kazi” alibainisha Rugemeleza
Akifungua mkutano huo jaji mstaafu Dkt .Fauz Twaib alisema kuwa mkutano huo utawawezesha wadau hao kushirikiana kwa pamoja na kuboresha njia bora zaidi za kutoa huduma.
“Kwa Sasa kumekuwa na wimbi kubwa la mawakili ,wametoka kwenye idadi mawakili Chini ya elfu moja miaka 10 iliopita na kufikia elfu 10 sasa katika hali ya aina iyo na upya wa mawakili wengi unasababisha changamoto kuwa nyingi Sana ,kwa ujumla kuna matukio mengi zaidi yanaoyoonekana kuonyeshwa Kuna aja ya kuangalia namna gani mawakili wanafanya kazi pamoja na maswala ya ueledi wao wa kufanya kazi”alibainisha Twaib
Akiongelea machapisho mbalimbali aliyoyazindua leo kwa ajili ya wanasheria alisema kuwa yatawasaidia kujua sheria mbalimbali ambazo hawazijui kwani hakuna mwanasheria ambaye anajua sheria zote papo kwa papo hivyo machapisho hayo yatamsaidia kujua kwa haraka kwani yamefupishwa.
Kwa upande wake wakili mstaafu Dkt Hawa Sinare alisema kuwa machapisho haya ni miongozo mzuri kwa wanasheria haswa wageni kwani itakuwa inawasaidia hata hawa wanasheria wachanga kujua Sheria ambazo walikuwa hawayajui.