*************************************************
Washiriki 20 wa shindano la Miss Tanzania 2020 leo wamemtembelea Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge ofisini kwake kwa lengo la kujitambulisha, kumsalimia na kupata Baraka za shindano hilo linalotaraji kufanyika siku ya kesho Disemba 05 kwenye ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere Jijini humo.
RC Kunenge amewapongeza washiriki hao kwa hatua waliyofikia na kuwataka kujiamini.