………………………………………………………………………….
Na.Ashura mohamed -Arusha.
Shirika lisilo la kiserikali la World Education Inc (WEI) kupitia mradi wa Waache wasome unaofadhiliwa na serikali ya Marekani limetoa Mafunzo kwa Waandishi wa habari 30 na walimu wa shule za Sekondari 261 katika jiji la Arusha.
Akizungumza wakati wa kufunga Mafunzo hayo Mkuu wa wilaya ya Monduli Edward Balele amewataka walimu kuhakikisha kuwa wanakuwa karibu na wanafunzi pamoja na kuhakikisha kuwa wanatumia mbinu mbadala katika kutekeleza adhabu mbali mbali.
Bw,Balele alisema kuwa ana Imani kuwa Mafunzo hayo yalitolewana WEI yatabadilisha mitizamo kwa walimu na kuwa mabalozi wazuri wa kupinga ukatili wa kijinsia miongoni mwa watoto.
‘’Hapa nimemuwakilisha mkuu wa mkoa wa Arusha ndugu yangu Hassan Kimanta na amenituma kuhakikisha kuwa haya mliofundishwa hapa mnakwenda kutekeleza ili mradi huu wa waaache wasome unatimiza lengo lake la kuhakikisha watoto wote wanapata elimu na tunatumia mbinu mbadala,ili kulinda haki za watoto’’alisema Balele
Aidha aliwataka walimu kuhakikisha kuwa wanatumia adhabu mbadala pamoja na kufuata maadili ya ualimu,ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wanakuwa katika mikono salama.
Alisema ili mradi huo uweze kuleta mageuzi makubwa,ni lazima walimu wawe mabalozi wazuri na kusimamia haki za watoto pamoja na kupinga vitendo vya kikatili hasa katika mazingira ya shuleni.
Grace Muro ambaye ni mkufunzi alisema kuwa wamewafundisha walimu Moduli sita ambazo zilitayarishwa na wizara tatu ambayo ni wizara ya maendeleo ya jamii jinsia na watoto,wizara ya elimu sayansi na teknolojia na wizara ya tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) ambapo Moduli hizo zipo mikonino mwa Tanzania Institute of Education (TAI).
Alisema kuwa Moduli hizo zimegawanyika katika maeneo mawili ambayo ni kufundishwa haki zao,wajibu wao na jinsi ya kujitambua na kubwa ni kufundisha waalimu kuacha ukatili wa kijinsia shuleni ambapo moduli hizi zipo sita.
“Moduli hizo ni pamoja na Haki za Mtoto na ile misingi sita ya haki za mtoto na sera,sheria ,miongozo ya serikali ambazo zinazungumzia haki za mtoto pamoja na mikataba ya mtoto,ikiwa ni pamoja na sheria za mtoto kuwa zinasemaje hivyo tumewafundisha walimu kuwa hawa watoto wanalindwa kisheria,Ukatili unavyoathiri mtoto na pia elimu iunaingiliana na jinsia hata hivyo aina za ukatikili hivyo walimu wameiva.”Bi,Muro alisema kuwa
Mmoja wa walimu hao kutoka Shule ya Sekondari Naura Dorcas Eliufoo alisema mafunzo hayo,yamewasaidia kubadili mbinu za ufundishaji pamoja na adhabu ambazo nyingine husababisha ukatili wa kijinsia kwa namna moja ama nyingine.