**************************************
~ Atatua kero kuu ya Soko
~ Atembelea eneo la mradi, aagiza ujenzi uanze ndani ya saa 24 kwa kasi kubwa
Na Mwandishi wetu Mihambwe
Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu amemaliza mgogoro kati ya kijiji cha Ng’ongolo na kijiji cha Miuta waliokuwa wakigombea umiliki wa soko ambapo amesimamia ipasavyo kuanzishwa kwa ujenzi wa soko jingine ambalo limeenda kuwa msuluhishi wa mgogoro huo ambapo sasa kila Kijiji kitakuwa na umiliki wa soko lake.
Gavana Shilatu alitembelea eneo la ujenzi mradi huo akiambatana na kamati za ujenzi mradi huo ambapo alikuta vifaa vya ujenzi vipo eneo la mradi na kuagiza ndani ya saa 24 ujenzi uanze mara moja.
“Suala la soko limekuwa kero na chanzo Cha matatizo. Nimeona vifaa vya ujenzi vipo site, natoa maelekezo ndani ya saa 24 ujenzi uanze mara moja na nitafuatilia kuona utekelezaji wake. Kamati simamieni mradi kwa uhakika ili thamani ya fedha iendane na mradi husika. Ukamilifu wa mradi huu utaenda kufuta kabisa mgogoro uliokuwepo, simamieni mradi ukamilike kwa wakati.” Alisisitiza Gavana Shilatu.
Katika ziara hiyo Gavana Shilatu aliambatana na kamati ya ujenzi mradi huo wa soko la kijiji cha Miuta pamoja na uongozi wa halmashauri ya Serikali ya Kijiji cha Miuta ukiongozwa na Mwenyekiti wa kijiji hicho