……………………………………………………………………….
Yamesalia Masaa Machache klabla ya kuanza kwa Semina na mafunzo makubwa ya mchezo wa Karate Tanzania (GASSHUKU 2020) ambayo yatakayofanyika Ruvuma(Songea) kuanzia 04/12/2020( Ijumaa) hadi 06/12/2020 (Jumapili).
Makarateka ambao Tayari wamewasili Ruvuma wameahidi kufanyia kazi mafunzo hayo Lengo la kuutangaza Mchezo wa Karate Tanzania pamoja na kuangalia viwango vya makarateka Nchini Tanzania.
Semina na mafunzo hayo yanayoandaliwa na Shirikisho la mchezo wa Karate Tanzania (JKA/WF-TZ) na itaongozwa na Mkufunzi mkuu wa Karate Tanzania Sensei Jerome Mhagama,pamoja na msaidizi wake Mikidadi Kilindo.
Sempai Kassim,ambaye ni mwanafunzi kutoka JKA HONBU DOJO (SCORPION) iliyopo Upanga Jijini Dar es salaam,ameelezea namna alivyojiandaa kwa mafunzo hayo,huku lengo lake likiwa ni kuwa mwalimu wa mchezo huo hapo Baadaye.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mh.Christina Solomon Mndeme anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi Katika Semina na mafunzo hayo,ambayo hunyika katika mikoa mbalimbali kila mwaka, baada ya mwaka jana kufanyika mkoani Morogoro,na mwaka huu mkoa wa Ruvuma ndiyo mwenyeji.