………………………………………………………………………….
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro ametoa siku 30, kukamilishwa kwa mradi wa maji wa zaidi ya shilingi bilioni 9 unaotekelezwa katika Halmashauri ya Arusha.
DC Muro, amefikia hatua hiyo ya kutoa siku 30, wakati wa ziara ya kazi ya kukagua miradi ya maji ambapo amesema mradi huo unapswa kukamilika ndani ya siku 30 ili wananchi wapate maji na salama ya kutumia ili kuondoka kero ya wananchi kwenda umbali mrefu kutafuta maji.
Mradi huu umelenga kusahidia vijiji vitano, vilivyo katia kata ya Ngaramtoni, Lemanyata na Oludonywasi ambapo wananchi zaidi ya 50,000 watanufaika.
Kati ziara ya hiyo ya ukaguzi wa maendeleo ya mradi huo, DC Muro ameambatana na Mkurugenzi wa halmashauri ya Arusha, Mbunge wa Arumeru magharibi, mwenyekiti mteule wa halmashauri ya Arusha, wadau Water Aid na watendaji wengine wa serikali na mamlaka za maji.
Mradi huu mkubwa unatekelezwa baina ya serikali ya Uingereza chini ya shirika la Water Aids na Serikali ya Tanzania.