Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji taka ,Mhandisi Lydia Ndibalema.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo akiwa ameambatana na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala Dk. Nkunga Daudi mwenye miwani wakati alipotembelea jengo la Jipya la Mama na Mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo akikagua baadhi ya vyumba vilivyopo katika jengo la Mama na Mtoto Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyama.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala Dk. Nkunga Daudi akitoa maelezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo eneo ambalo litatumika kwa ajili kutolea huduma ya CT- SCANI katika jengo jipya ya la Mama na Mtoto.Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo akijaribu kifaa cha mashine ya mfumo wa kupumulia alipotembelea jengo jipya la Mama na Mtoto.
********************************************
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo ameupongeza uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala kwa kusimamia vizuri ujenzi wa Jengo jipya la kisasa la Mama na Mtoto litakalo anza kutoa huduma hivi karibuni.
Akizungumza wakati alipofanya ziara katika Hospitali hiyo, Mhe. Chongolo amesema kuwa jengo hilo ambalo limejengwa kwa fedha za Serikali litakuwa mahususi kwa Wananchi wa maeneo yote yaliopo ndani na nje ya Manispaa hiyo kwa kuwa litatoa huduma nyingi ambazo awali hazikuwepo.
Ameongeza kuwa kukamilika kwa hatua za mwisho kwa jengo hilo kutatoa fursa ya huduma za upimaji kwa kutumia CT-SCAN, Privante Room, kitu ambacho awali hakikuwepo Hospitalini hapo na kwamba Wananchi watapata huduma hiyo kwa ufanisi mkubwa.
Aidha Mhe. Chongolo amesisitiza kuwa mara baada ya kukamilika kwa maandalizi hayo ambayo yatakamilika baada ya wiki mbili, atarejea kuhakiki na hivyo kuruhusu huduma hizo kuanza kutolewa na kwamba Serikali inafanya kazi kubwa katika kuhakikisha kuwa Wananchi wanapata huduma iliyo bora.
“ Nimefurahishwa na kazi nzuri ambayo imefanyika, ninawapongeza kwa namna ambavyo mnashirikiana kuhakikisha kwamba matumizi ya jengo hili yana anza rasmi, nitarudi tena kujiridhisha katika maandalizi ya jumla kabla ya kuanza kulitumia hili jengo jipya la huduma ya mama na Mtoto” amesema Mhe. Chongolo.
Nakuongeza kuwa” nategemea matokeo kwa haraka ili wale ambao wanapata huduma ya Afya katika Hospitali yetu ya Rufaa ya Mkoa, Mwananyamala waanze kupata huduma iliyobora, Serikali ya Rais Dk. Magufuli inafanya kazi kubwa, imetoa fedha nyingi kiasi cha Bilioni 2.2 kwa ajili ya Hospitali hii kuboresha huduma inahitaji pia kuona matokeo ya haraka.
Awali Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala Dk. Nkungu Daudi amempongeza Mhe. Chongolo kwakuwa karibu wakati wa ujenzi wa Hospitali hiyo na kusema kwamba jengo hilo limekamilika kwa silimia 98 na kwamba kinachosubiriwa hivi sasa ni kuunganishwa kwa umeme kwenye jengo pamoja na mfumo wa majitaka wa jamii iliuanze kutumika.
Ameongeza kuwa katika jengo hilo kutakuwa na vitanda, 78 kwa ajili ya watu wazima, Watoto wa changa, Wodi ya Mama na Mtoto,Mama wajawazito, huduma za kujifungulia, sambamba na wale wanaohitaji huduma za Privece.
“Hospitali hii itakuwa na mambo mengi ya kitaalamu ambayo yapo kwa mfumo wa kisasa zaidi, kutakuwa na utoaji wa huduma za kibingwa ,tunamabingwa zaidi 24 katika Hospitali yetu ,inawezekana walikuwa wanashindwa kuja kutokana na kukosa huduma hiyo lakini hivi sasa zitakuwepo” amesema Dk. Nkunga.