Wakili Sylvester Temu akiongea na wanahabari hawapo pichani kwenye banda la Kampuni hiyo mapema leo kwenye kongamano la wanasheria TLS linalofanyika kwenye Hotel ya Lush Garden wilayani Arumeru picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha
Bango linaloonyesha mfano wa kadi kwa ajili ya kupata huduma kwa njia ya mtandao wa tehama kama ilivyokutwa na kamera ya matukio kwenye banda ya kampuni hiyo mapema leo wilayani Arumeru.
Familia bora baada ya kuandika wosia kama inavyoonekana kwenye Bango la kampuni ya ABC ATTORNEY kwenye viwanja vya hotel ya Lush Garden wilayani Arumeru mapema leo picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha
……………………………………………………………………………
Na Ahmed Mahmoud Arusha
Kampuni ya ABC ATTORNEYS yenye makazi yake jijini Dar es Salaam imezindua huduma ya tehama kwa kadi za kieletroniki kwa wateja wake itakayosaidia kupata huduma bila kufika ofisini kwao.
Akiongea mapema leo mwakilishi wa kampuni hiyo wakili Sylvester Temu kwenye maonyesho yalioenda sambamba na kongamano la siku Tatu la chama cha wanasheria Tanganyika TLS ameeleza
kuwa upo umuhimu na faida ya kuwa na kadi hizo.
Alisema kuwa kadi hizo zine faida kwa kumsaidia mteja wao kujua mwenendo wa maendeleo ya kazi aliyoipatia kampuni tena kwa muda wowote na mahali popote nchini.
Kwa mujibu wa wakili Temu kadi hizo pia inasaidia mteja wetu kupata points na baadae kufanikiwa kufanyiwa kazi bila malipo pindi atakapokuwa mteja kwa muda.
Faida nyingine ni mteja wetu kuweza kufanya mawasiliano na wanasheria wake bila kufika ofisini kwetu.
Akizungumzia suala la kuandika wosia wakili Temu alisema kuwa utoaji wa mafunzo ya kuandika wosia ili kuwa na furaha katika familia pia wosia unasaidia kulinda familia yako na kulinda Mali yako.
Alisema bado kwenye suala la kuandika wosia kumekuwa na changamoto kwa jamii kudhani kuwa wakiandika basi ndio watakufa hilo halina ukweli wosia humsaidia mteja kulinda mali zake na familia yake.