……………………………………………………………….
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge ameonyesha kutoridhishwa na zoezi la majaribio ya uchinjaji wa Ng’ombe na Mbuzi kwenye machinjio ya kisasa Vingunguti baada ya kubaini kasoro za uendeshaji wa mtambo hiyo.
Miongoni mwa kasoro alizobaini RC Kunenge ni pamoja kukosekana kwa utaalamu wa uendeshaji wa mitambo, Zoezi la uchinjaji kutumia muda mrefu kuanzia hatua ya Kwanza Hadi mwisho, kukwamakwama kwa vifaa kwa baadhi ya maeneo, Kazi nyingi kufanywa na binadamu badala ya mashine Na wafanyakazi kufanya kazi kwa kubahatisha jambo lililopelekea Ng’ombe mmoja kutumia zaidi ya nusu saa Hadi kukamilika badala ya dakika 10.
Kutokana na hayo RC Kunenge amemtaka Mkandarasi wa ufungaji wa mashine, Mshauri wa Mradi, NHC na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kufika ofisini kwake Alhamis ya Disemba 3 saa nne asubuhi.
Aidha RC Kunenge amewaelekeza NHC kuongeza kasi ili Ujenzi wa jengo ukamilike kwa wakati huku akimuelekeza Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kuwa mkali.
Pamoja na hayo RC Kunenge amemtaka Mkandarasi wa ufungaji wa mitambo kuhakikisha anatoa elimu ya matumizi ya mitambo kwa wafanyakazi ili waweze kuzitumia.