……………………………………………………………..
Na Masanja Mabula, Pemba.
MAHAKAMA ya Mkoa Chake Chake imempleka rumande kwa muda wa wiki mbili mtuhimiwa Issue Foum Machano anayetumiwa kwa kosa la mauaji.
Mtuhumiwa huyo mwenye umri wa miaka 55 anadaiwa kumuuwa aliyekuws askari wa vikosi vya SMZ.
Mbele ya hakimu wa mahakama hiyo Luciano Makoye ,mwendesha mashaka wa serikali Juma Ali Juma aliniambia mahakama kwamba mtuhumiwa huyo ametenda kosa hilo siku ya tarehe 28/19/2020 majira ya saa 2 usiku.
Amesema siku ya tukio huko Ngwachani Mkoàni,alimuuwa askari huyo Khalfan Juned Mohammed jambo ambalo ni kosa kisheria.
Alisema kuwa kosa hilo ni kinyume na kifungu Cha 179 na 180 Cha sheria ya adhabu namba 6 ya mwaka 2018 sheria za serikali ya Zanzibar.
Hata hivyo mtuhumiwa huyo hakutakiwa kujibu lolote kwani mahakama hiyo haina uwezo kisheria wa kusikiliza kesi za aina hiyo.
Kesi hiyo imepangwa kusikiliza terehe 15 /12/2020 katika mahakama ya juu Pemba.