Mkuu wa Mkoa wa Geita Eng. Robert Gabriel pamoja na Mkuu wa Mkoa Shinyanga Bi. Zainab Telack wakikagua mabanda ya maonesho ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika viwanjwa vya Butulwa nje kidogo ya Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Eng. Robert Gabriel akiwa na Mkuu wa Mkoa Shinyanga Bi. Zainab Telack pamoja naye Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Bi. Yasinta Mboneko wakikagua mabanda ya maonesho ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika viwanjwa vya Butulwa nje kidogo ya Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Eng. Robert Gabriel pamoja na Mkuu wa Mkoa Shinyanga Bi. Zainab Telack wakikagua mabanda ya maonesho ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika viwanjwa vya Butulwa nje kidogo ya Mkoa wa Shinyanga.
Badhi ya Wananchi wa Manispaa ya Shinyanga wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Geita Eng. Robert Gabriel hayuko pichani wakati wa ufunguzi wa maonesho ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika viwanjwa vya Butulwa nje kidogo ya Mkoa wa Shinyanga.
……………………………………………………………………………………………………
Na Anthony Ishengoma-Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zainab Telack amewataka wawekezaji katika sekta ya madini kuwekeza katika Mkoa wa Shinyanga badala ya kuja kuchuma mali za mkoa huo na kwenda kuwekeza katika mikoa mingine tofauti na Shinyanga.
Bi. Telack amewahakikishia wafanyabiashara katika sekta ya madini kutokuwa na wasiwasi kuwekeza Shinyanga na kuwahakikishia uhakika wa uwepo wa fursa ya ardhi ya uwekezaji na kuonya kuwa kushindwa kuwekeza Shinyanga kunaufanya Mkoa huo kuendelea kuwa Shamba la Bibi.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga amesema hayo jana wakati wa hotuba yake kwa wananchi wa Mkoa huo wakati wa kufungua Maonesho ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika viwanja vya Butulwa vilivyopo nje kidogo ya Manispaa ya Shinyanga.
“Mnakuja kuchuma Shinyanga na kuondoka na mamilioni ya Shinyanga, wengine wananiambia Shinyanga haina biashara, biashara inawezeshwa na watu wekezeni katika mkoa wenu, mnachuma na kuondoka mnatarajia nini na wengine ni wazawa wa Mkoa huu pendeni Mkoa wenu.” Alisisitiza Mkuu wa Mkoa B. Zainab Telack.
Bi. Telack alitaja faida ya Maonesho hayo kuwa ni kuwaezesha wafanya biashara kujifunza fursa za masoko, kupata masoko ya Madini ikiwemo kujifunza teknolojia mpya ya madini lakini pia kuepukana udaganyifu wakati wa kufanya biashara ya madini akiongeza kuwa pia ni fursa kwa wachimbaji wadogo kupata elimu ya soko la madini lilipo mkoa wa Shinyanga.
Bi. Telack amewataka wawekezaji wenye nia ya kuanzisha kiwanda cha Vito vya thamani kama mikufu na kukata almasi kufanya hivyo mara moja kutokana na upatikanaji kwa wingi wa madini ya dhahabu pamoja na almasi.
Aidha Bi. Telack amewataka wamiliki wa migodi mikubwa ikiwemo Mgodi mkubwa wa almasi wa Mwadui na Barick Gold mine kuwekeza na kuendeleza eneo la Butulwa ambalo ni eneo la kimkakati la biashara na kuhaidi kuwapatia eneo ili wawekezaji miundombinu ya kudumu kwa ajili ya maonesho ya teknolojia ya madini kwani eneo hilo kuanzia sasa litaendelea kutumika kufanyia maonesho ya madini na fursa za kilimo mkoani Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Eng. Robert Gabriel Mgeni rasmi wa Maonesho hayo alisema fursa za Maonesho hayo ni masoko akiitaja fursa hiyo kuwa muhimu kwani inawakutanisha muuzaji na mnunuzi.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa wa Geita alisema faida ya kuanzishwa kwa masoko ya madini ni kuzuia utoroshaji wa madini pamoja na kurahisisha ulipaji wa Kodi za Serikali.
Eng. Gabriel aliongeza kuwa kupitia maonesho hayo wachimbaji wadogo wa madini wanapata fursa ya kujua idadi ya masoko iliyopo Mkoa wa Shinyanga lakini kuwawezesha wawekezaji kujua mahitaji halisi ya wateja wao.
Maonesho ya Teknolojia ya Madini Mkoani Shinyanga ni ya kwanza nay a aina yake kufanyika Mkoani Shinyanga na yamekuwa yakiendelea tangu Novemba 25 na Kilele cha Maonesho hayo ni tarehe 1 Desemba, 2020.