Mbunge wa Makete Mhe.Festo Sanga akiongea na wahitimu wa chuo cha ufundi VETA Makete pamoja na wazazi wakati wa sherehe za mahafali ya sita ya chuo hicho.
Mgeni rasmi kwenye mahafali ya sita ya chuo cha ufundi VETA(mwenye suti nyeusi)ambaye ni Mbunge wa jimbo la Makete Mhe.Festo Sanga akipata maelezo kutoka kwa wanafunzi wa chuo hicho juu ya shughuli wanazofanya.
*************************************
Na Mwandishi wetu,Makete
MBUNGE wa jimbo la Makete Festo Sanga amehaidi kuwasomesha vijana 10 kila mwaka katika chuo cha ufundi VETA Makete huku akiwataka wazazi kupeleka vijana wao kwa wingi katika chuo hicho ili waweze kujifunza fani mbalimbali.
Sanga ameyasema hayo kwenye akiwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya sita ya chuo cha ufundi VETA Makete
“Kwakweli inasikitisha kuona kati ya wanafunzi 64 wanaohitimu leo, wanafunzi wanaotokea hapa Makete hawafiki 10, zaidi ya 50 wanatoka nje ya Makete Mara, Tukuyu, Tanga, Dar es Salaaam, Iringa na Mikoa mingine tafsiri yake ni kushindwa kuitumia fursa ya kusomesha watoto wetu hapa sisi wanamakete, nawaomba sanaaa tuwalete vijana wetu hapa waje wasome, Serikali imewekeza mabilioni ya fedha katika chuo hiki pekee cha VETA Mkoani kwetu”alisema Sanga
Alisema mitambo iliyopo chuoni hapo haipatikani katika vyuo vingine vya VETA kirahisi.
“Kwa kuanza, mimi kama Mbunge wenu hapa nitakuwa nasomesha wanafunzi 10 kila mwaka kutoka maeneo mbalimbali ya kata zetu ndani ya Makete ambao wanauhitaji na wanamazingira Magumu ya kiuchumi”alisema
Sanga alisema kwenye mikutano yake yote atazungumzia kuhusu chuo cha n VETA cha Makete kwani ada zake ni nafuu na watanzania wengi wanaouwezo wakuzimudu.
Kwa upande wao wanafunzi waliokuwa wakihitimu chuoni hapo wameomba kuongezwa kwa kozi nyingine kama kozi za ufundi bomba,mapishi,umeme wa magari na majumbani na zingine ili iwasaidia kupata watalaam wengi na hiyo itafanya wanafunzi kuchagua kitu anachopenda kusomea tofauti na sasa wanasomea vitu ambavyo hawajavichagua.
Kaimu Mkuu wa Chuo cha VETA Makete Xavier Meta amesema kwasasa wamejipanga kuongeza zaidi madarasa manne ambayo yatasaidia kupunguza msongamano wa wanafunzi na kuongeza udahili zaidi,ujenzi wa maktaba ambao utasaidia zaidi ufaulu mzuri kwa wanafunzi.
“Chuo chetu sasa hivi kimejipanga katika ujenzi wa miundombinu kama madarasa,maktaba ili kuepuka adha ya msongamano wanaopata,pia tuweze kudahili wanafunzi wengi wakusoma hapa.