Mgeni Rasmi mkuu wa mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel, akizungumza kwenye maonyesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini mkoani Shinyanga.
Eneo la maonyesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini mkoani Shinyanga, lililopo eneo la Butulwa Kata ya Old -Shinyanga.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, akisoma taarifa kwenye maonyesho hayo ya Biashara na Teknolojia ya Madini.
Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi, akisoma taarifa ya maonyesho hayo ya Biashara na Teknolojia ya Madini.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini Patrobas Katambi, akizungumza kwenye maonyesho hayo ya Biashara na Teknolojia ya Madini mkoani Shinyanga.
Mwenyekiti wa Chemba ya wafanyabiashara na viwanda mkoani Shinyanga Meshack Kulwa, akitoa shukrani kwenye maonyesho hayo ya Biashara na Teknolojia ya Madini.
Mkuu wa mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel, (wa tatu kutoka kulia) akizindua maonyesho ya Biashara na Tekno
lojia ya madini mkoani Shinyanga, wapili kulia ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, wa kwanza kushoto ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akifuatiwa na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini Patrobas Katambi.
Mkuu wa mkoa wa Geita Robert Gabriel, kulia, akiwa kwenye Banda la Tume ya Madini, akiwa ameshika madini ya Almasi.
Zoezi la ukaguzi wa mabanda likiendelea kwenye maonyesho hayo ya Biashara ya Teknolojia ya Madini.
Zoezi la ukaguzi wa mabanda likiendelea kwenye maonyesho hayo ya Biashara ya Teknolojia ya Madini.
Zoezi la ukaguzi wa mabanda likiendelea kwenye maonyesho hayo ya Biashara ya Teknolojia ya Madini.
Zoezi la ukaguzi wa mabanda likiendelea kwenye maonyesho hayo ya Biashara ya Teknolojia ya Madini.
Na Marco Maduhu- Shinyanga.
MKUU wa mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel, amezindua rasmi maonyesho ya biashara na Teknolojia ya madini mkoani Shinyanga, na kuwataka wawekezaji wa madini kwenda kuwekeza mkoani humo, ili kuunyanyua mkoa huo kichumi na kukua kimaendeleo.
Uzinduzi wa maonyesho hayo umefanyika leo Jumamosi Novemba 28,2020 katika eneo la Butulwa Kata ya Old Shinyanga manispaa ya Shinyanga, na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa madini, akiwemo na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini Patrobas Katambi na Elias Kwandikwa wa Ushetu, ambayo yatakoma Desemba Mosi mwaka huu.
Akizungumza kwenye maonyesho hayo, mkuu wa mkoa wa Geita, ameupongeza mkoa wa Shinyanga kwa kuanzisha maonyesho hayo, ambayo yatakuwa ni chachu kubwa ya kukuza uchumi wa mkoa huo.
“Naupongeza sana mkoa wa Shinyanga kwa kuanzisha maonyesho haya ya Biashara na Teknolojia ya madini, ambayo ni muhimu sana katika kutangaza fursa za uwekezaji, pamoja na wawekezaji wadogo wa madini kujifunza namna ya kutumia Teknolojia za kisasa za kuchimba madini na kupata mali nyingi,” amesema Gabriel.
“Pia nawaomba wawekezaji wakubwa wa migodi mkoani Shinyanga, mtoe kipaumbele kwa wazawa katika ajira za migodini, ikiwamo na kusambaza bidhaa mbalimbali ndani ya migodi hiyo ili wapate kunufaika na rasilimali za nyumbani na siyo kutoa ajira kwa watu wanje,”ameongeza.
Katika hatua nyingine ameitaka migodi hiyo mikubwa kuwekeza miradi mikubwa ya kiuchumi mkoani Shinyanga, ambayo itaacha alama na kuleta maendeleo ili kuubadilisha mkoa huo kimaendeleo na kuendana na hadhi ya rasirimali ilizonazo, na siyo kuwaachia mashimo na umaskini mkubwa.
Naye mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, amesema wameanzisha maonyesho hayo ya biashara na Teknolojia ya madini, ili kutoa fursa kwa wawekezaji na wafanyabiashara kuwekeza mkoani humo kwa sababu ni mkoa ambao una madini mengi.
Amesema katika mauzo ya Almasi kuanzia Julai 2020 hadi Novemba, wameuza Almasi zaidi ya Shilingi Bilioni 42.5, hivyo haoni sababu ya mkoa huo kuendelea kuwa maskini.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Geoffrey Mwangulumbi, amesema wazo hilo la kuanzisha maonyesho hayo lilianza mwaka 2017 hadi 2019, mara baada ya kufanya utafiti, na kuona Shinyanga imedumaa kimaendeleo kwa sababu ya kukosekana kwa mzunguko wa kifedha
Aidha amesema maonyesho hayo ya Biashara na Teknolojia ya madini yatakuwa yakifanyika kila mwaka mwezi Julai, ili kuongeza thamani ya mnyororo katika Sekta ya madini na kuuinua kiuchumi mkoa wa Shinyanga.