Home Mchanganyiko FORVAC YAWAPA MBINU WAANDISHI  KUADIKA HABARI ZA UCHUNGUZI  ZA MISITU ZINAZOHUSU MISITU 

FORVAC YAWAPA MBINU WAANDISHI  KUADIKA HABARI ZA UCHUNGUZI  ZA MISITU ZINAZOHUSU MISITU 

0
Mratibu wa Program ya Mnyororo wa Thamani wa Mazao ya Misitu (FORVAC), Emmanuel Msoffe akizungumza na waandishi wa habari wanaoshiriki mafunzo kuhusu misitu, mazingira na uhifadhi wilayani Ruangwa mkoani Lindi.
Waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo kuhusu misitu, mazingira na uhifadhi yaliyoandaliwa na Program ya Mnyororo wa Thamani wa Mazao ya Misitu (FORVAC) yanayofanyika wilayani Ruangwa mkoani Lindi.
*****************************************
NA SULEIMAN MSUYA, RUANGWA
PROGRAM ya Mnyororo wa Thamani wa Mazao ya Misitu (FORVAC) imetoa mafunzo kwa waandishi wa  habari zaidi ya 20 kutoka vyombo na mikoa mbalimbali kuhusu uandishi wa Habari za Kiuchunguzi za Kimisitu (IJF) kwenye sekta ya misitu ili kuchochea uhifadhi na  maendeleo.
Mafunzo hayo yametolewa na wakufunzi Cassin Sianga na Deo Mfugale kupitia  Programu ya FORVAC  ambayo inatekelezwa na Idara ya Misitu na Nyuki chini ya  Wizara ya Maliasili na Utalii .
Akizungumza baada ya ufunguzi wa mafunzo hayo Mratibu wa Kitaifa wa FORVAC, Emmanuel Msoffe amesema wamekuwa wakitoa mafunzo kwa waandishi wa habari ili kuwajengea uelewa kuhusu programu hiyo na misitu kwa ujumla kwa ajili ya kuelimisha umma juu ya manufaa ya uhifadhi endelevu wa misitu.
Msoffe amesema wanaamini  kuwa waandishi wakiwa na uelewa wa faida na  thamani iliyopo kwenye misitu na  mazao yake misitu kiuchumi, kijamii, kimazingira  na  maendeleo  endelevu wataweza kuandika habari nzuri za kiuchunguzi za misitu na kusaidia Serikali katika kufikisha ujumbe chanya kwa wananchi kuhusu uhifadhi.
“Kumekuwepo jitihada za kuhamasisha Usimamizi Shirikishi wa Misitu ya Jamii (USMJ), hivyo FORVAC imeamua kuja na program hii ili kufanikisha dhana nzima ya uhifadhi endelevu wa misitu  na tunaamini kupitia nyie waandishi mabadiliko  makubwa yatapatikana hivi karibuni  kwa kasi,” amesema
Msoffe amesema Tanzania ina zaidi hekta milioni 48.1 za misitu ambapo hekta milioni 21.6  zipo katika misitu ya vijiji ila takiribani hekta milioni 2.4 ndizo zimehifadhiwa na vijiji. Waandishi wanapaswa kuandika kwa kina adhari za kukosekana uhifadhi ili Serikali na wadau wengine wajitokeze kufanya USMJ.
Mratibu huyo amesema hadi sasa FORVAC imenufaisha zaidi ya watu  wadau 330,000 katika Kongani za  Lindi, Ruvuma na Tanga na kwamba matamanio yao ni watu wengi kufikiwa.
“FORVAC ina malengo ya kuongeza  thamani ya mnyororo wa kwenye mazao ya misitu kama mbao, mkaa  asali na mengine  yanayopatikana msituni huku misitu ikiwa endelevu,” amesema.
Mshauri wa kiufundi  wa FORVAC, Tanzania Juhani Härkönen amesema wanaridhishwa na mafanikio yanayopatikana katika wilaya 12 zilizopo kwenye program hiyo inayotarajiwa kuisha 2022.
Ametaja baadhi ya Wilaya hizo kuwa ni Handeni Kilindi, Kiteto na Mpwapwa, Ruangwa, Nachingwea, Liwale, Tunduru Namtumbo,  Mbinga, na Nyasa, Mpwapwa, Handeni na Kilindi.
“Tunaamini FORVAC itachochea USMJ ila watu wa kuonesha matokeo chanya au hasi katika program hii ni nyinyi waandishi, na sisi tumedhamiria kuchochea mabadiliko hayo,” amesema.
Kwa upande wake Ofisa Maliasili wa Mkoa wa Lindi Zawadi Jilala , amesema mkoa unaungana na FORVAC pamoja na taasisi nyingine ambazo zimejikita kwenye uhifadhi wa misitu kwa njia endelevu.
Amesema mkoa huo unazaidi ya hekta 900,000 za misitu ambayo ipo kwenye vijiji 70 hivyo ili kuifanya iwe endelevu wanahitajika wadau mbalimbali kushirikiana nao.
Joseph  amesema mafanikio mengine ambayo yamepatikana kupitia miradi ya USMJ ni pamoja na mpango wa matumizi bora ya ardhi.
Wakufunzoi Sianga na Mfugale waliwataka waandishi hao zaidi ya 23 kujikita kwenye uandishi wa kiuchunguzi wa misitu  ili waweze kuibua mambo mazuri na mabaya yanatokea hasa katika sekta ya misitu.
Wamesema habari za uchunguzi zinahitaji muda, kujituma, kujiamini na kuweka maslahi ya umma mbele.
“Habari za uchunguzi zinahitaji kujituma kweli sio lelemama tunaamini hadi mwisho wa program tutakuwa na asilimia 20 ya wanaofanya habari hizi,” amesema.