******************************
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATUHUMIWA 32 KWA TUHUMA ZA MAKOSA MBALIMBALI YAKIWEMO YA KUVUNJA NYUMBA USIKU NA KUIBA, WIZI WA BAJAJI NA PIKIPIKI, KUPATIKANA NA BHANGI NA KUPATIKANA NA POMBE MOSHI @ GONGO.
KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA WA KUVUNJA NYUMBA USIKU NA KUIBA.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kuanzia tarehe 20.11.2020 liliendesha msako katika maeneo ya Mwanjelwa, Soweto, Mwakibete, Mwambene, Mama John, Iyela, Mtaa wa Kagera – Ilomba, Iganzo na Sinde Jijini Mbeya dhidi ya wahalifu wa matukio ya kuvunja nyumba usiku na kuiba, wizi wa bajaji na pikipiki, kupatikana na bhangi na kupatikana na pombe moshi @ gongo.
Katika misako hiyo watuhumiwa sita [06] wa matukio ya kuvunja nyumba usiku na kuiba pamoja na wizi wa Bajaji na Pikipiki walikamatwa wakiwa na mali mbalimbali za wizi ambao ni:-
- RAISON MWENGA [26] Mkazi wa Iyela.
- VICTOR RICHARD MWASHIGALE [38] Mkazi wa Makunguru.
- DAUD MWANG’ITA [20] Dereva Bajaji na Mkazi wa Iganzo.
- BEATUS ANDREA [28] Mkazi wa Uyole.
- JAMES CHARLES [27] Mkazi wa Airport ya zamani
- THOMAS ANDREA [22] Mkazi wa Airport ya zamani
Baada ya kuhojiwa, watuhumiwa hao walikiri kuhusika na matukio ya uvunjaji nyumba nyakati za usiku na kuiba mali mbalimbali na kueleza mahali walipohifadhi vitu hivyo. Kikosi kazi cha Jeshi la Polisi cha kuzuia na kupambana na uhalifu Mkoa wa Mbeya kilifika mpaka maeneo walipoficha mali hizo na kufanikiwa kupata vitu vifuatavyo:-
- TV moja aina ya Sundar inchi 32.
- Ds Player aina ya Winning Star,
- Redio ndogo na begi dogo.
- Baiskeli mbili bambucha,
- Godoro mbili,
- Blanketi moja,
- Ovena aina ya Nikai na Kenwood,
- Dovet moja,
- Spika mbili aina ya Boss,
- Meza ya TV,
- Kompyuta Desk Top aina ya Dell,
- Keyboard moja,
- CPU aina ya HP,
- Majiko ya Gesi matano aina ya Oryx, Mtungi mdogo wa gesi aina ya Oryx,
- Jiko la kupikia plate mbili,
- Sukari kilo 11,
- Radio Sub-Woofer na Spika mbili aina ya Pinteck, Radio Sub-Woofer aina ya Seapiano, Radio ndogo aina ya Sundar,
- Begi kubwa la nguo, Begi la kike na vikoba vidogo vitatu.
- Remote Control 6,
- Bisibisi tatu.
Sambamba na hilo, watuhumiwa hao walikiri kuiba bajaji yenye namba za usajili MC 747 CMV aina ya TVS rangi nyeusi huko maeneo ya Mianzini Kata ya Mwakibete na kwenda kuificha maeneo ya Iganzo na baadae walikwenda kuiuza Mkwajuni Mkoa wa Songwe. Mmiliki wa bajaji hiyo ameitambua, taratibu za kumkabidhi zinaendelea.
Aidha wakati msako huo ukiendelea Jeshi la Polisi mkoani hapa lilifanikiwa kupata Pikipiki yenye namba za usajili MC 922 BMZ aina ya Kinglion rangi nyekundu iliyoibiwa huko Soweto mwezi Juni 2020.
Upelelezi wa mashauri hayo unaendelea na mara baada ya kukamilika watuhumiwa watafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.
KUPATIKANA NA BHANGI.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa sita [06] kwa tuhuma za kupatikana na dawa za kulevya aina ya Bhangi kete 30 sawa na uzito wa gramu 150.
Watuhumiwa hao walikamatwa katika msako uliofanyika tarehe 25.11.2020 majira ya saa 20:00 usiku huko maeneo ya Ilolo, Kata ya Sinde, Tarafa ya Sisimba, Jijini Mbeya. Watuhumiwa waliokamatwa ni pamoja na:-
- NOSHA NDOMBA [27]
- MESHACK TITO [19]
- ALEX MWALIYOYO [25]
- JUMA WHITE [18]
- MUSTAFA WHITE [22]
- ALLY WHITE [24] wote wakazi wa Isanga.
Watuhumiwa ni wauzaji na watumiaji wa bhangi. Taratibu za kuwafikisha mahakamani zinaendelea.
KUFUNGWA KWA WATUHUMIWA WATATU KWA MAKOSA YA KULAWITI NA KUBAKA.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limefanikiwa kuwafunga jela watuhumiwa watatu wa makosa ya kubaka na kulawiti. Watuhumiwa waliofungwa ni pamoja na:-
- SAID MRISHO [21] Mkazi wa Chunya ambaye amefungwa jela kifungo cha Maisha baada ya kukutwa na hatia kwa kosa la kumlawiti mtoto wa kiume wa miaka 07. Mtuhumiwa alikamatwa huko Kijiji cha Mazimbo tarehe 20/03/2020 na kufikishwa Mahakama ya Wilaya ya Chunya CC NO.77/2020.
- JAMES ALIKO PONDO [27] Mkazi wa Chunya ambaye amefungwa jela miaka 30 baada ya kukutwa na hatia kwa kosa la kumlawiti mtoto wa kiume wa miaka 10. Mtuhumiwa alikamatwa tarehe 05/02/2020 huko katika Kijiji cha Kibaoni na kufikishwa Mahakama ya Wilaya ya Chunya CC NO.39/2020.
- FADHIL MWAMBAPA [28] Mkazi wa Chunya ambaye amefungwa jela miaka 30 baada ya kukutwa na hatia kwa kosa la kubaka mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 13. Mtuhumiwa alikamatwa tarehe 18/04/2020 na kufikishwa Mahakama ya Wilaya ya Chunya CC NO.102/2020.
WITO WA KAMANDA.
Ninatoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana kwa karibu na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za viashiria vya uhalifu, wahalifu kupitia namba zetu za simu za mkononi ili tuweze kushughulika na wahalifu. Aidha ninatoa rai kwa wananchi walioibiwa mali zao kama vile TV, Mitungi ya Gesi pamoja na Pikipiki kufika kituo kikuu cha Polisi Mbeya wakiwa na nyaraka za uthibitisho wa kumiliki mali hizo kwa ajili ya utambuzi na kufanya taratibu za kurejeshewa mali zao.
Aidha naendelea kutoa wito kwa watendaji wa Kata na Mitaa kuhakikisha wanashirikiana na Polisi Kata waliopo katika maeneo yao, kuhakikisha wanaunda vikundi vya ulinzi shirikishi kwa ajili ya kufanya doria katika maeneo yao. Sambamba na hilo niendelee kuwakumbusha watendaji na wamiliki wa nyumba za kupanga kuhakikisha wana watambua wageni wanaoingia katika maeneo yao kwa ajili ya usalama wao na mali zao.