Home Michezo MAELFU WAMZIKA DIEGO MARADONA KWENYE MAKABURI YA BELLA VISTA

MAELFU WAMZIKA DIEGO MARADONA KWENYE MAKABURI YA BELLA VISTA

0

NYOTA mkubwa wa soka, Diego Maradona amezikwa jana katika zoezi lililoshuhudiwa na maelfu ya mji Mkuu wa Argentina, Buenos Aires.
Jeneza lake lilisindikizwa na ulinzi mkali kutoka Ikulu, Casa Rosada kwenda makaburi ya viwanja vya Bella Vista, ingawa haikuzuia watu kuruka uzio na kuonyesa hisia zao kwa ishara tofauti.
Mabinti wa Maradona, Dalma mwenye umri wa miaka 33, na Giannina miaka 31 aliyezaa na mke wake wa kwanza na mpenzi wake utotoni, Claudia Villafane walionekana wakifuta machozi wakati wakiondoka mazishini. 
Maradona alifariki dunia Jumatano kwa matatizo ya moyo nyumbani wake, Buenos Aires, ambako alikuwa amepumzika baada ya kufanyiwa upasaji wa ubongo Novemba 3.
Diego Maradona amezikwa jana katika zoezi lililoshuhudiwa na maelfu ya mji Mkuu wa Argentina, Buenos Aires PICHA ZAIDI SOMA HAPA
Barani Ukaya, utaratinu wa kusimama kimya kwa dakika moja kabla ya mechi kuanza ulianza kwenye michuano ya UEFA Europa League kutoa heshima kwa Diego Maradona, aliyefariki dunia Jumatano akiwa ana umri wa miaka 60.