Home Michezo ARSENAL YAICHAPA 3-0 MOLDE FK NA KUTINGA 32 BORA EUROPA LEAGUE

ARSENAL YAICHAPA 3-0 MOLDE FK NA KUTINGA 32 BORA EUROPA LEAGUE

0

Arsenal imefanikiwa kutinga hatua ya 32 Bora michuano ya Europa League baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya wenyeji Molde FK, mabao ya  Nicolas Pepe dakika ya 50, Reiss Nelson dakika ya 55 na Folarin Balogun dakika ya 83 usiku wa jana Uwanja wa Aker Stadion, Molde. Arsenal inafikisha pointi 12 baada ya ushindi huo kufuatia kucheza mechi nne na kuendelea kuongoza Kundi B kwa pointi sita zaidi ya Molde na Rapid Wien, huku Dundalk, timu nyingine kundini ikiwa haina pointi PICHA ZAIDI SOMA HAPA