Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto anayeshughulikia Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Dkt. John Jingu akizungumza katika kongamano la Wataalamu wa Jamii lililofanyika jijini Mwanza.Mwenyekiti wa TASWO Dkt.Mariana Makuu akizungumza katika kongamano la Wataalamu wa Jamii lililofanyika jijini Mwanza.
************************************
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto anayeshughulikia Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Dkt. John Jingu amehitimisha kongamano la Wataalamu wa Jamii lililofanyika jijini Mwanza.
Dkt. Jingu ametumia fursa hiyo kutoa rai kwa Chama cha Wataalamu wa Ustawi wa Jamii Tanzania (TASWO) kusimamia miiko ya wataalamu hao ili kuhakikisha wanatikiza vyema majukumu yao.
Naye Mwenyekiti wa TASWO, Dkt. Mariana Makuu amepongeza ushirikiano unaotolewa na Serikali kwa Wataalamu wa Ustawi wa Jamii wakati wa kushughulikia majanga mbalimbali ikiwemo janga la hivi karibuni la Covid 19 (Corona) ambapo wataalamu hao walishiriki katika hatua zote.
“Pia tunampongeza Rais Dkt. John Magufuli kwa namna alivyotuongoza kwenye mapambano dhidi ya Corona, tuliondoa hofu katika jamii na kwa uwezo wa Mungu tukashinda” amesema Makuu.