Mkuu
wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kulia akipokea msaada wa komputa
mbili na printa moja zilizotolewa na Benki ya Posta (TPB) wenye thamani
ya milioni 3.5 kutoka kwa Mkurugenzi wa Fedha wa Benki hiyo Regina
Semakafu kwa ajili ya ofisi ya Ardhi Mkoa wa Tanga
Mkuu WA Mkoa wa Tanga Martine Shigella kulia akipokea msaada wa komputa

BENKI
ya Posta imetoa msaada wa vitendea kazi kompyuta mbili na printa moja
zenye thamani ya milioni 3.5 kwa ajili ya ofisi ya Ardhi mpya Mkoa wa
Tanga ikiwa ni sehemu yao ya kuisaidia jamii katika kutatua changamoto
mbalimbali.
Akizungumza wakati akikabidhi msaada huo,Mkurugenzi
wa Fedha wa Benki hiyo Regina Semakafu alisema msaada huo ni wajibu wao
kama benki wakiwa wanaihudumia jamii hivyo wakaona umuhimu wa kuisaidia
jamii katika kukutana na changamoto mbalimbali.
Alisema kwamba
wanaamini hivyo vifaa ambavyo wamevitoa vitasaidia kuwahudumia wananchi
na kupunguza changamoto za ofisi mpya ya ardhi mkoa wa Tanga .
“Hivyo
tunaamini vifaa tulivyovitoa leo vitasaidia kuwahudumia wananchi na
kupunguza changamoto za ofisi mpya ya ardhi mkoa wa Tanga “Alisema
Mkurugenzi huyo wa Fedha.
Awali akizungumza mara baada ya
kupokea hivyo,Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella aliishuku Benki
hiyo kwa msaada huo ambao wameutoa kwa ajili ya ofisi ya ardhi mkoa huo.
Alisema kwamba kama wanavyofahamu serikali ya awamu ya tano
inayoongozwa na Dkt John Magufuli imejipambanua kwenye kufanya maboresho
na kutatua changamoto za ardhi katika Taifa letu.
Mkuu huyo wa
mkoa alisema ardhi inachangamoto nyingi sana na kwa mkoa huo hivyo
anafarijika kuona kwamba ofisi imefunguliwa ikiwa inahitaji mahitaji
mengi ikiwemo upatikanaji wa thamani na vifaa kama ambavyo
vimekabidhiwa.
“Hivyo niwaambie kwamba mmekuja wakati muafaka
kusawaidia na kuwapatia huduma watumishi wetu wa ofisi ya ardhina vifaa
hii sio kwamba watavitumia kwa maslahi yao bali ni kwa maslahi ya
wananchi wa mkoa wa Tanga “Alisema RC Shigella.
Hata hivyo
aliwaishukuru benki hiyo kwa msaada huo huku akieleza kwamba ni
matumaini yake kuona vifaa hivyo vinatunza na ili viweze kudumu na
kupata thamani.
“Lakini niwaambie wananchi wa mkoa watembelea
ofisi ya ardhi wapate hati na waweze kuzitumia kwa ajili ya kukopa na
eneo pekee ni benki ya posta lakini wafungue akaunti zao kwenye benki
hiyo”Alisema RC Shigella.