Madiwani wateule 31 wa wilaya ya Karagwe wakila kiapo kabla ya kuanza kutekeleza majukumu yao katika mkutano wa kwanza wa Halmashauri ambao ni mahsusi kwa ajiri ya viapo, kuchagua viongozi wa halmashauri na uundaji wa kamati mbalimbali za halmashauri baada ya kushinda katika uchaguzi mkuu uliofanyika mnamo Oktoba 28,2020, kiapo hicho kimetolewa na Hakimu msaidizi wa mahakama ya wilaya ya Karagwe Bi. V. M Mushi. Leo, Novemba 26,2020(Picha na Eliud Rwechungura)
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya karagwe na Diwani wa kata ya Nyaishozi, Mhe. Wallace Mrokozi Mashanda akiomba kura za ndio za kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Karagwe katika mkutano wa kwanza wa Halmashauri ambapo amechaguliwa kwa kura zote 32 za ndio zilizopigwa na Madiwani na Mbunge wa jimbo la karagwe. Leo, Novemba 26,2020(Picha na Eliud Rwechungura)
Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya karagwe na Diwani wa kata ya Rugera, Mhe. Dawson Paul Byamanyirwohi akiomba kura za ndio za kuchaguliwa kuwa makamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Karagwe katika mkutano wa kwanza wa Halmashauri ambapo amechaguliwa kwa kura zote 32 za ndio zilizopigwa na Madiwani na Mbunge wa jimbo la karagwe. Leo, Novemba 26,2020(Picha na Eliud Rwechungura)Mbunge wa jimbo la Karagwe, Mhe. Innocent Bashungwa akiongea na madiwani na kuwasilisha vipaumbele vya utekelezaji wa maendeleo kwa madiwani katika mkutano wa kwanza wa Halmashauri ambao ni mahsusi kwa ajiri ya viapo kwa madiwani, kuchagua viongozi wa halmashauri na uundaji wa kamati mbalimbali. Leo, Novemba 26,2020(Picha na Eliud Rwechungura).
***************************************
Madiwani wateule 31 wa wilaya ya Karagwe wamekula kiapo kabla ya kuanza kutekeleza majukumu yao katika mkutano wa kwanza wa Halmashauri ambao ni mahsusi kwa ajiri ya viapo na kuchagua viongozi wa halmashauri na uundaji wa kamati mbalimbali za halmashauri baada ya kushinda katika uchaguzi mkuu uliofanyika mnamo Oktoba 28,2020, kiapo hicho kimetolewa na Hakimu mkuu wa wilaya ya Karagwe Bi. V. M Mushi
Madiwani walioapishwa ni kama ifuatavyo; Mhe. Ladislaus Kamuhangire, Diwani kata ya Ihanda, Mhe. Wallace Mahanda, Diwani kata ya Nyaishozi, Mhe.Shadrack Ntimba, Diwani kata ya Ndama, Mhe.Dawson Byamanyirwohi, Diwani kata ya Rugera, Mhe.Adrian Kobushoke, Diwani kata ya Rugu, Mhe.Charles Bechumila, Diwani kata ya Nyakahanga, Mhe.Magnus Cheusi, Diwani kata ya Kibondo, Mhe.Chrian Pastory, Diwani kata ya Igurwa, Mhe.Thomas Rwentabaza, Diwani kata ya Nyabiyonza, Mhe.Mugisha Mathias, Diwani kata ya Bugene, Mhe.Levina Kibogoyo, Diwani kata ya Ihembe, Mhe. Anord Rwenseleka, Diwani kata ya Chonyonyo, Mhe.Xavery Buguzi, Diwani kata ya Nyakakika, Mhe.Justine Fidelis, Diwani kata ya Nyakabanga, Mhe.Rwamuhangi Mugasha, Diwani kata ya Kihanga, Mhe.Fidel Belebe, Diwani kata ya Kamagambo, Mhe. Mzakiru Mussa, Diwani kata ya Bweranyange, Mhe. Valensi Kasumuni, Diwani kata ya Nyakasimbi, Mhe.Longino Rwenduru, Diwani kata ya Chanika, Mhe. Evarister Sylvester, Diwani kata ya Kiruruma, Mhe.Tayebwa Murishid, Diwani kata ya Kituntu, Mhe. Frolian Rwamafa, Diwani kata ya Kanoni, Mhe.Germanus Byabusha, Diwani kata ya Kayanga, Mhe. Jane Bilaro, Diwani viti maalum kata ya Nyaishozi, Mhe.Prisca Busenene, Diwani viti maalum kata ya Kibondo, Mhe.Genegeva Busenene, Diwani viti maalum kata ya Kituntu, Mhe. Anitha Richard, Diwani viti maalum kata ya Nyaishozi, Mhe.Jovitha Kombe, Diwani viti maalum kata ya Nyabiyonza, Mhe.Edina Mugashe , Diwani viti maalum kata ya Chanika, Mhe.Siima Ezekiel, Diwani viti maalum kata ya Ihembe, Mhe. Joyce Aenda, Diwani viti maalum kata ya Kayanga.
Kulingana na shughuli katika mkutano wa kwanza wa Halmashauri ambao ni mahsusi kwa ajiri ya kuchagua viongozi wa halmashauri, Mwenyekiti wa kikao na Katibu tawala wa wilaya ya Karagwe Ndg. Innocent Nsena ameongoza uchaguzi wa kuwachagua Mwenyekiti wa halmashauri na makamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya karagwe ambapo Diwani wa kata ya Nyaishozi, Mhe. Wallace Mrokozi Mashanda amechanguliwa kuwa mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya karagwe kama mgombea pekee kwa kura zote 32 za ndio, pia amechaguliwa Diwani wa kata ya Rugera, Mhe.Dawson Paul Byamanyirwohi kuwa makamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Karagwe kama mgombea pekee kwa kura zote 32 za ndio zilizopigwa na madiwani na Mbunge wa jimbo la Karagwe, Mhe. Innocent Bashungwa.
Aidha, Mbunge wa Jimbo la Karagwe, Mhe. Innocent Bashungwa amepata nafasi ya kuongea katika mkutano huo na ameaanza kwa kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa ushindi wa kishindo alioupata katika uchaguzi mkuu uliofanyika hivi karibuni, pia amaekishukru Chama Cha Mapinduzi na Madiwani wote kwa kuamini na wanannchi na kuwatuma kuwawakilisha katika baraza la madiwani, Samabamaba na hao amempngeza msimamizi wa uchaguzi na mkurugenzi wa wilaya ya Karagwe kwa kusimamia uchaguzi ulioisha amabao umekuwa huru na wa haki ambao umepelekea Chama Cha Mapinduzi kushinda viti vya udiwani 22 kati ya 23 kwa wilaya ya Karagwe.
Sambamba na hayo Bashungwa amepata kuwasilisha vipaumbele vya maendeleo kwa madiwani ambavyo vitafanyiwa kazi haraka iwezekanavyo ili kuhakikisha ahadi walizozitoa katka kampeni zinatekelezwa kwa haraka na ndani ya muda mfupi na kuhakikisha ilani ya Chama Cha Mapinfuzi ya 2020 -2025 inatekelezwa kwa asilimia 100 bila kujali kata yenye diwani kutoka upinzani.