*************************************
Na John Walter-Manyara
Mkurugenzi mtendaji wa Tume ya sheria na Haki za Binadamu Tanzania (LHRC) Bi. Anna Henga amewasihi wananchi kutokubali kufanya au kufanyiwa Ukatili wa kijinsia na kuwasaidia wanaofanyiwa vitendo hivyo ili kufikia haki.
Henga amesema endapo jamii itakubali kupinga vitendo hivyo kwa nguvu, itasaidia kuokoa wengi wanaotendewa vitendo hivyo na hatimaye kubaki salama.
Amezungumza hayo novemba 25,2020 akizungumza kwa njia ya simu na kituo cha redio cha Smile Fm kilichopo Mjini Babati mkoa wa Manyara kuhusu Siku 16 za kupinga Ukatili wa Kijinsia Duniani.
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimeanza maadhimisho hayo Novemba 25 ambapo Novemba 30 watakutana Wanawake watetezi wa Haki za Binadamu na kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kutoa tuzo kwa Wanawake huku Desemba 10 wakihitimisha kwa kutoa Tuzo,Mafunzo,Semina na Warsha.
Henga amesema licha ya kuwepo kwa changamoto, uelewa umeongezeka kwa Jamii kuelewa Haki zao mbalimbali kwa kujua wapi pa kuelekea endapo amefanyiwa ukatili.
Amesema awali hapakuwa na Madawati ya Jinsia ambapo kwa sasa yapo katika vituo vya Polisi na watu wanayafahamu huku zitungwa sera na miongozo mbalimbali ya Jinsia imeboreshwa na kamati zimeundwa kwa ajili ya kupinga Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto.
Ameyataka ambayo bado maeneo yanawafanyia Ukeketaji Wanawake na Watoto kuacha tabia hizo akiutaja mkoa wa Manyara kama kinara wa kitendo hicho ambacho ni kosa Kisheria pamoja na haki za binadamu.
Kauli Mbiu ya mwaka 2020 ‘Tupinge Ukatili wa Kijinsia: Mabadiliko Yanaanza na Mimi’.