MABINGWA watetezi, Bayern Munich wamejihakikishia kwenda Hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa baada ya ushindi wa 3-1 dhidi ya RB Salzburg katika mchezo wa Kundi A usiku wa jana Uwanja wa Allianz Arena Jijini Munich. Mabao ya Bayern Munich yalifungwa na Robert Lewandowski dakika ya 42, Maximilian Wober aliyejifunga dakika ya 52 na Leroy Sane dakika ya 68, wakati la RB Salzburg lilifungwa na Mergim Berisha dakika ya 73. Bayern Munich inafikisha pointi 12 na kuendelea kuongoza kundi hilo kwa pointi saba zaidi ya Atletico Madrid, wakati RB Salzburg inaendelea kushika mkia kwa pointi yake mmoja, nyuma ya Lokomotiv Moscow yenye pointi tatu kuelekea mechi za mwisho PICHA ZAIDI SOMA HAPA