…………………………………………………………………………..
Na.Mwaandishi Wetu,Dar es Salaam.
Mabingwa wa Kihistoria Tanzania bara Yanga wamepanda kileleni mwa Msimamo wa Ligi Kuu Vodacom baada ya kuichapa bao 1-0 Azam FC katika uwanja wa Chamazi Complex nje kidogo ya jijini La Dar es salaam.
Timu zote mbili zilianza kushambuliana kwa zamu kipindi cha kwanza na kupelekea kwenda mapumziko zikiwa hazijafungana huku Yanga wakiwa wametawala mchezo kwa kukosa nafasi mbili za wazi.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko huku zikishambuliana kwa zamu huku kosa kosa zikitawala kwa timu ya Yanga.
Shujaa wa Yanga alikuwa Deus Kaseke mnamo dakika ya 48 akipokea pasi kutoka kwa Mshambuliaji Yacouba Songne aliweza kuitumia vizuri na kumuacha Mlinda mlango wa Azam FC David Kisu hana la kufanya.
Kwa ushindi huo Yanga wamepanda kileleni kwa kufikisha pointi 28 na kuwaacha Azam FC katika Nafasi ya pili wakiwa na pointi 25.
Matokeo Mengine ya leo Ruvu Shooting wameichapa 1-0 Tanzania Prisons,Kagera Sugar wakiwa uwanja wao wa Nyumbani wameichapa 3-0 Biashara United toka Musoma na Gwambina FC wakiwa ugenini wamepata ushindi wa mabao 4-3.