**************************************
Na Rahel Nyabali Kigoma.
Serikali ya mkoa wa kigoma imeitaka mamlaka ya maji mjini na vijijini RUWASA kuhakikisha inakamilisha kwa ubora sitahiki miradi ya maji katika vijiji ishirini na mbili .
Akizindua miradi hiyo ya maji mkuu wa mkoa wa kigoma Tobius Ndengenye wilayani Buhigwe ,amesema miradi inaogharimu kiasi cha zaidi shiringi bilioni 20 kwa mkoa mzima ambao miradi hiyo imefadhiliwa na Serekali ya Ubirigiji kwa Ushilikiana Serekaliya Tanzania na kusisitiza kukamilika kwa mradi mapema ili wanchi waondokane na adha ya maji.
Mhandisi wa maji Ruwasa mkoani kigoma Matias Mwenda ameahidi kusimamia kikamilifu ma kumtaka mkandarasi wa Kampuni ya Seregeti limited kukamilisha kwa kwa wakati .
Mkuu wa wilaya ya buhigwe Kanali Michael Ngayalina amewasisitiza wananchi kutunza miundombinu ya maji kwani miradi mingi katika maeneo mbalimbali imekuwa ikitumika kwa mda mfupi kasha kuharibika.
Hatahivyo wananchi walio pata miradi hiyo akiwemo Tamasha Athumani na Adamu Makuka wameshukuru Serekali kwa kuwaletea miradi hiyo na kuahidi kulinda miundombinu ya miradi ya maji.