Meneja Mauzo wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam – Tumaini Alila akimkabidhi fulana mia moja Afisa Habari wa Manispaa ya Ilala – Tabu Shaibu kwa ajili ya Siku ya Mlipa Kodi. Wakishuhudia ni; a pili kutoka kulia ni Mweka Hazina wa Manispaa ya Ilala – Tulusubya Kamalamo ( wapili kushoto), Meneja Mahusiano Biashara na Serikali wa NMB – Mkunde Joseph (Kulia) na Afisa Mahusianoa Tawi la NMB Morogoro Road- Adelaida Mirisho. Mweka Hazina wa Manispaa ya Ilala – Tulusubya Kamalamo akionyesha fulana walizo kabidhiwa na Benki ya NMB kwa ajili ya Siku ya mlipo Kodi. Wengine ni Meneja Mauzo wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam – Tumaini Alila(Wapili kushoto) Meneja Mahusiano Biashara na Serikali wa NMB – Mkunde Joseph (Kulia) na Afisa Mahusianoa Tawi la NMB Morogoro Road- Adelaida Mirisho.
***********************************
Kongamano la Siku ya Mlipa Kodi Manispaa ya Ilala, limefunguliwa leo Jumatano Novemba 25, huku Benki ya NMB ikisapoti kwa kukabidhi fulana (T-shirt) 100 zenye thamani ya Sh. Mil. 1.1 za kuvaa washiriki wa warsha iliyoambatana na ufunguzi huo.
Hafla ya ufunguzi wa Tamasha la Siku ya Mlipa Kodi Manispaa ya Ilala, imefanyika katika Ukumbi wa Anatoglo, Mnazi Mmoja, kisha ikifuatiwa na warsha na semina mbalimbali, ikiwemo kuhusu Kodi ya Huduma iliyotolewa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Mkoa wa Ilala.
Akizungumza wakati akikabidhi fulana 100 kwa washiriki wa Tamasha hilo, Meneja Mauzo wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Tumaini Alila, alisema msaada huo umelenga kuunga mkono jitihada za Serikali kufikisha Elimu ya Mlipa Kodi kwa jamii ya Kitanzania.
“NMB tunatambua umuhimu wa kulipa kodi thamani ya jitihada hizi za Serikali kusambaza elimu hii kwa jamii ili kuwa na Taifa linalojali na kuzingatia ulipaji Kodi. Hii ndio Siri iliyotusukuma kusapoti kongamano hili kwa Manispaa ya Ilala,” alisema Tumaini.
Meneja huyo aliyekabidhi msaada huo kwa niaba ya Benki ya NMB, alibainisha kuwa maendeleo ya Taifa lolote yanawategemea walipa Kodi na wao kama NMB licha ya kuwa walipa Kodi vinara serikalini, wanajisikia fahari kuona elimu kwa Mlipa Kodi inamfikia kila mmoja ili awe sehemu ya maendeleo ya nchi yake
Kwa upande wake, Adeltus Kazinduki, ambaye ni Ofisa Mtendaji Kata ya Kipawa, kwa niaba Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, aliipongeza NMB kwa namna inavyounga mkono harakati za Serikali katika nyanja mbalimbali.
Kongamano la Siku ya Mlipa Kodi Manispaa ya Ilala, lililojumuisha walipa Kodi na mamlaka mbalimbali za Serikali zikiwemo Takukuru, TRA nk, linatarajia kufungwa kesho Alhamisi Novemba 26, kuhitimisha siku mbili za elimu kwa njia ya warsha na semina za elimu ya ulipaji Kodi.