……………………………………………………………………………………….
NJOMBE
Madiwani waliopita katika Uchaguzi mkuu uliofanyika octoba 28 mwaka huu kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi wilayani Ludewa mkoani Njombe wamefanya uchaguzi wa ndani ya chama wa nafasi ya mwenyekiti,makamu na katibu wa baraza la madiwani ambao wanakwenda kuchuana na chama cha ACT na CHADEMA katika uchaguzi wa kuwapata viongozi wa baraza la madiwani la halmashauri hiyo.
Kabla zoezi la upigaji kura kuanza Mkuu wa wilaya ya Ludewa Andrea Tsere na Horas Kolimba mwenyekiti wa CCM wilayani humo wakatoa rai kwa wapiga kura kuhakikisha wanarusu akili kufanya maamuzi badala ya mionyo ili kuwapata viongozi watakaokuwa mstari wa mbele kupigania maslahi ya umma.
Mara baada ya uchaguzi kufanyika msimamizi Bakari Mfaume akawatangaza washindi wa uchaguzi huo wa ndani ambo unakwenda kuchuana na wawakilishi wa vyama pinzani viwili ambavyo vimeshinda kata 3 kati ya 26 zilizopo mwambao mwa ziwa nyasa wayani humo.
Grace Mapunda na Dominic Mganwa na Joseph Kamonga ambaye ndiye mbunge Mteule wa Ludewa wanasema wanaimani baraza la sasa litakuwa bora zaidi kwasababu linamchanganyiko wa vyama na kwamba linakwenda kutoa kipaumbele katika migodi ,barabara,elimu,Kilimo na afya.
Katika Uchaguzi huo Charles Mgina ameshinda nafasi ya mwenyekiti kwa kura 19 dhidi ya Lezile Haule mwenyekiti mstaafu,Nafasi ya makamu mwenyekiti akishinda Leodiga Mpambalyoto huku katika nafasi ya katibu akipitishwa Daniel Muhagama 18 na Katibu msaidizi Michael Haule 14.